Gavana wa Nairobi Mike Sonko apendekeza Miguna Miguna awe naibu gavana

Chanzo cha picha, @MIGUNA MIGUNA/TWITTER
Gavana wa mji mkuu wa Kenya Nairobi Mike Mbuvi Sonko amependekeza mwanasaisa wa upinzani anayekumbwa na utata Miguna Miguna kuwa naibu gavana.
Bw Sonko alitoa tangazo hilo ambalo halikutarajiwa siku ya Jumatano jioni kwa njia ya barua kwa spika wa bunge la kaunti ya Nairobi, akisema Miguna Miguna ametimiza matakwa yote yanayohitajika kikatiba.
Barua hiyo imekuwa ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii na kuzua maoni mengi kutoka kwa Wakenya, kutokana na kuwa uteuzi wake umekuja wakati ambao haukutarajiwa.
Aidha, Bw Miguna amekuwa mkosoaji mkuu wa gavana huyo na kabla ya uchaguzi alisema Bw Sonko hana sifa zozote za uongozi na hawezi kuliongoza jiji la Nairobi.
Miguna ambaye ana uraia wa Canada na Kenya, alitarajiwa kurudi nchini Kenya kutoka Canada baada ya kutimiliwa na serikali, lakini akaahirisha safari yake akisema kuwa idara ya uhamiaji huikumpa pasipoti halali jinsi ilivyoagizwa na mahakamma.

Chanzo cha picha, AFP/GETTY IMAGES
Alitajarajiwa kuwasili Nairobi tarehe 16 mwezi huu licha ya kutimuliwa kutoka Kenya na serikali mara mbili katika kipindi cha miezi mitatu.
Alikuwa arudi nyumbani siku ambayo barua ya kuteuliwa kwake inaaminiwa kuandikwa.
Nafasi ya naibu gavana ilibaki wazi kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa naibu gavana Polycarp Igathe tayehe 12 Januari mwaka huu, kwa kile alichokitaja kuwa gavana kukosa kuwa na imani kwake kuhusu kusimamia masuala ya kaunti.
Bw Igathe kwa sasa ameteuliwa kuwa mmoja wa maafisa wa wakuu wa benki ya Equity, moja ya benki kubwa zaidi Kenya.
Spika wa Bunge la Kaunti ya Nairobi Beatrice Elachi amesema Bw Miguna atahitajika kutatua masuala kuhusu uraia wake na serikali ya Kenya kabla yake kuhojiwa na wabunge wa jimbo hilo.
Bw Miguna anahitaji kuidhinishwa na bunge hilo kabla yake kuidhinishwa rasmi kuchukua wadhifa huo.
"Gavana ametupa jina la aliyempendekeza. Tutafuata sheria. Katiba iko wazi kwamba naibu gavana anahitaji kuwa raia wa Kenya. Ningemshauri Miguna kwamba kwanza atatue matatizo yake na serikali ya Kenya. Yeye ni raia wa Canada. Shughuli hii itatuchukua miezi mitatu hadi minne," Bi Elachi alisema katika kituo cha redio cha Hot 96 FM.
Tayari kuna utata kuhusu iwapo ataidhinishwa baadhi ya wanasiasa wakikosoa uteuzi huo.
Seneta wa Nairobi Johnson Sakaja ameandika kwenye Twitter kwamba mwanasiasa huyo "hawezi kuwa naibu gavana wa Nairobi".
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Kufikia sasa, bw Miguna hajazungumzia hatua hiyo ya Bw Sonko.
Baadhi ya Wakenya mtandaoni wameunga mkono hatua hiyo lakini wengine wanapinga, kama wakili huyu Ahmednasir Abdullahi.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
Seneta wa Makueni Mutula Kilonzo Jr anaamini Spika wa Nairobi Bi Elachi hahitaji ufafanuzi wowote kuhusu uraia wa Bw Miguna.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 3