Stormy Daniels amshtaki Trump juu ya ujumbe wa Twitter

Trump at press conference

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 2

Mwigizaji wa filamu za ngono Stormy Daniels amemshtaki Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu ujumbe wa Twitter anaodai ni wa kumharibia jina, wakili wake amesema.

Bi Daniels, ambaye jina lake halisi ni Stephanie Clifford, anasema alitishiwa na mwanamume mmoja katika maegesho ya magari mjini Las Vegas na kutakiwa kuacha kuendelea na madai yake kwamba aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Bw Trump.

Rais huyo wa Marekani alipakia kwenye Twitter mchoro wa mwanamume mshukiwa na kisha kuandika "hii ni kazi ya utapeli kabisa".

Wakili wa Bi Daniel aliandika kwenye Twitter kwamba Bw Trump "anafahamu vyema kabisa yaliyotokea".

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

"Bw Trump alitumia fursa ya mamilioni ya watu katika taifa hili na kimataifa (wanaomfuatilia katika mtandao huo wa kijamii) kutoa taarifa ya uongo yenye lengo la kumshushia hadhi na kumshambulia Bi Clifford," kesi iliyowasilishwa katika mahakama ya dola mjini New York inasema.

Stormy Daniels, seen here with her lawyer Michael Avenatti, outside a federal court in Manhattan talking to reporters

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Stormy Daniels akiwa na wakili wake Michael Avenatti

Kesi hiyo inasema ujumbe huo wa rais ulikuwa wa kumharibia mtu jina kwani ulimtuhumu Bi Daniels kwa "kutekeleza kosa kubwa" - hususan, la kumtuhumu mtu mwingine kwamba alimtishia.

Bw Trump alikuwa amepakia mtandaoni mapema mwezi huu picha ya mchoro wa mshukiwa huyo na kumweleza kuwa "mwanamume asiyekuwepo".

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

Bi Daniels anasema yeye na rais huyo walikuwa na uhusiano wa kimapenzi kuanzia 2006.

Bw Trump amekanusha tuhuma hizo.

Mwanamke huyo aliambia kipindi cha CBS News kwamba baada ya kutamatika kwa uhusiano wao, mwanamume mmoja alifika alipokuwa yeye na binti yake katika maegesho hayo ya magari Las Vegas na kumwambia "sahau taarifa hiyo, mwache Donald Trump".

Bi Daniels awali alimshtaki wakili wa Bw Trump, Michael Cohen, akitaka kuvunjwa kwa mkataba wa kutofichua siri kuhusu uhusiano huo, ambao anasema Bw Trump hakuutia saini.

Bw Cohen awali alikiri kwamba alimpa Bi Daniels $130,000 zake mwenyewe, lakini alisema kwamba hakueleza ni kwa nini alitoa pesa hizo.

Michael Cohen photographed as he arrives at the US Courthouse in New York on April 26, 2018

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Trump amekana kuwa na ufahamu wowote kumhusu Cohen ambaye hapa anaonekana akiingia mahakamani

Kesi hiyo hata hivyo ilisitishwa kwa siku 90, huku jaji akisema kwamba haki za Bw Cohen zingekuwa hatarini iwapo kesi hiyo ingeendelea akiwa bado anachunguzwa.

Bw Cohen anachunguzwa na Mwanamashtaka Maalum Robert Mueller kuhusu tuhuma kwamba Urusi iliingilia uchaguzi wa urais wa mwaka 2016 na kwamba taifa hilo lilishirikiana na maafisa wa kampeni wa Rais Trump.