Maelfu ya Waislamu wa Rohingya waliuawa Myanmar mwezi mmoja pekee

Two-year-old Hazera, confused and scared, holds on to her mother after reaching Bangladesh from Myanmar
Maelezo ya picha, Miongoni mwa wakimbizi hao, kuna watoto wengi

Shirika la Madaktari waso na Mipaka (MSF) limesema watu takriban 6,700 wa jamii ya Rohingya waliuawa katika mwezi ambao makabiliano yalizuka Myanmar mwezi Agosti.

Kwa kutumia utafiti uliofanywa miongoni mwa wakimbizi Bangladesh, maafisa wa shirika hilo wanasema idadi hiyo ni ya juu mno kuliko idadi rasmi iliyotangazwa na serikali ya Myanmar ambayo ni 400.

MSF wamesema hiyo ni "ishara ya karibuni zaidi ya jinsi ukatili huo ulivyoenea".

Jeshi la Myanmar limewalaumu "magaidi" kutokana na vita na mauaji hayo na limesema halifai kulaumiwa.

Watu zaidi ya 647,000 wa jamii ya Rohingya wamekimbilia Bangladesh kama wakimbizi tangu Agosti, MSF wamesema.

Utafiti wa shirika hilo ulibaini kwamba takriban watu 9,000 wa jamii ya Rohingya walifariki nchini Myanmar, taifa ambalo pia hufahamika kama Burma, kati ya 25 Agosti na 24 Septemba.

Miongoni mwa waliofariki, MSF wanasema, 730 ni watoto wa chini ya miaka mitano.

Jeshi limekiri kwamba watu 400 waliuawa, wengi ambao lilisema walikuwa magaidi wa Kiislamu.

Rohingya
line

Jeshi lilianza operesheni ya kukabiliana na wapiganaji wa Arsa wa Rohongya baada ya wanamgambo hao kushambulia zaidi ya vituo 30 vya polisi.

Baada ya uchunguzi wa ndani, jeshi la Myanmar mwezi Novemba lilijiondolea lawama.

Jeshi hilo lilikanusha kuwaua raia, kuchoma vijiji, kuwabaka wanawake na wasichana na kupora mali.

Wengi wa watu wa jamii ya Rohingya ambao ni Waislamu hunyimwa uraia Myanmar na hutazamwa kama wahamiaji kutoka Bangladesh.

An injured Rohingya boy lifts his T-shirt to reveal a large bandage across his stomach
Maelezo ya picha, MSF wanasema mengi ya wanayosema walipitia Warohingya ni ya kusikitisha

Serikali huwa haitumii jina Rohingya bali huwaita Waislamu wa Bengal.

Momtaz Begum

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Wengi wa wakimbizi hao walitendewa ukatili