Wakimbizi 35,000 wa Rohingya kutoka Myanmar wawasili Bangladesh ndani ya saa 24

Chanzo cha picha, Reuters
Idadi ya watu wa jamii ya Rohinhya wanaovuka kutoka Myanmar na kuingia nchini Bangladesh imeongeka kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa huku zaidi ya watu 35,000 wakiwasili ndani ya saa 24 zilizopita.
Zaidi ya watu 123,000 wanaripotiwa kukimbia ghasia katika jimbo la Rakhine nchini Myanbar tangu tarehe 25 mwezi Agosti mwaka huu.
Mzozo huo uliibuka wakati wanamgambo wa Rohingaya walishambulia vituo vya polisi.

Chanzo cha picha, Reuters
Hii ilisababisha jeshi kuingilia kati hatua ambayo imesababisha maelfu ya watu wa Rohingaya kuhama vijiji vyao.
Jamii ya Rohingya ni watu wasio na uraia ambao wamekubwa na na mateso nchini Myanmar. Wengi wa wale ambao wamehama wamesema kuwa jeshi linachoma vijiji vyao na kuwashambulia raia katika harakati za kuwatimua.

Jeshi linasema kuwa linawapiga vita wanamgambo wa Rohingya ambao wanawashambulia raia.
Umoja wa Mataiafa unasema kuwa haijulikani hasa ni lini wakimbizi hao waliingia Bangladesh, lakini umesema kuwa idadi ya wakimbizi wapya wanaohitaji chakula na makao inaongezeka kwa haraka.

Chanzo cha picha, Mir Sabbir/BBC








