Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ubakaji wa mtoto wa miaka 6 ulioitamausha India
Polisi nchini India wanawahoji watu kadhaa kufuatia kisa cha ukatili cha ubakaji wa mtoto wa miaka sita katika jimbo la kaskazini mwa nchi la Haryana.
Mwili wake ulipatikana Jumapili karibu na kwenye nyumba yao ambapo alidaiwa kutekwa usiku wa tarehe 8 mwezi Disemba.
Kiwango cha majeraha ya mtoto huyo kimewatamausha watu nchini India,
Mamayake mtoto huyo aliiambia BBC kuwa kile wanataka ni haki.
"Yamepita masaa 24 na bado polisi hajamshika yeyote," alisema.
Polisi wamewakamata watu watatuakutoja kwa familia ya mume wake kuhojiwa lakini hakuna mtu alishikwa hadi sasa.
Serikali imebunia kikosi cha uchunguzi kufuatia shinikizo kutoka kwa mamlaka ili kuwakamata wale waliotekeleza kitendo hicho.
Wenyeji wakiwemo wanaharakati na viongozi wa kisiasa wamekusanyika katika kijiji hicho kuandamana.