Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mwathiriwa wa ubakaji wa miaka 13 India aiomba mahakama kutoa mimba
Wazazi wa msichana mwenye umri wa miaka 13 mwathiriwa wa ubakaji kutoka mji wa Mumbai huko India, wamekwenda katika mahakama kuu ya nchi hiyo, kuomba idhini ya kutoa mimba aliyo nayo binti wao.
Msichana huyo ana mimba ya wiki 30.
Sheria nchini India, inakubalia utoaji mimba wa wiki 20 ikiwa tu maisha ya mama yamo hatarini.
Mimba hiyo iligunduliwa baada ya wazazi wake kumchukua kwa daktari kwa matibabu, kutokana na kuongezeka uzito kupita kiasi.
Msichana huyo anasema kuwa alibakwa na rafiki wa babake, ambaye kufikia sasa amekamatwa na kuzuiliwa.
Kesi hiyo inafanyika siku kadhaa baada ya msichana mwingine mwathiriwa wa ubakaji mwenye umri wa miaka 20, kujifungua katika mji ulioko Kaskazini mwa India wa Chandigarh.
Masaibu yake yaliwagusa wengi kote duniani huku vyombo vya habari vikiangazia pakubwa taarifa hiyo, hasa baada ya mahakama kukatalia mbali ombi la kutoa mimba hiyo kwamba mimba hiyo ilikuwa ni imezidisha muda.
Mwezi Mei, kesi kama hiyo iliripotiwa katika mji wa Hyarana kaskazini mwa India, ambapo msichana mwenye umri wa miaka 10 ambaye alidaiwa kubakwa na babake wa kambo, alikubaliwa kuitoa mimba hiyo.
Mwaandishi wa BBC mjini Delhi huyo India, Geeta Pandey, anasema kuwa kesi tatu kama hiyo, imewashangaza wengi, lakini wanaharakati wanaamini kuwa, kuna uwezekano wa visa vingi kama hivyo, ambavyo haviripotiwi na vyombo vya habari, kwa sababu vinagunduliwa baada ya makataa ya majuma 20 na wazazi wengi hawaripoti visa kama hivyo kwa polisi.
Visa hivi vitatu viligonga vichwa vya habari, kwa sababu viliangaziwa wakati muda umemalizika- kwani watoto hao wenyewe wa kike hawakufahamu hali yao.
Wazazi wao pia walikosa kuona dalili na uja uzito, kwa sababu hawakuamini kwam,ba wasichana wao wameshika mimba katika umri mdogo hivyo, mwaandishi wetu ameongeza.
'Hatari ya kiafya'
Hivi ndivyo ilivyokuwa kwa kisa cha msichana wa miaka 13, mtalamu wa masawala ya wanawake mjini Mumbai Dkt Nikhil Datar, ameiambia BBC.
"Aliletwa kwangu na wazazi wake mnano Agosti 9, walishuku kuwa anugua ugonjwa wa tezi, kwa sababu alikuwa akiongezeka unene. Baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu alipatikana kuwa na mimba ya wiki 27, na hapo ndipo walipofahamisha maafisa wa polisi," alisema.
Mbali na msichana wa miaka 10, ambaye alifichwa kuwa ana mimba huku akidanganywa kuwa uvimbe alio nao tumboni ni jiwe ndani ya tumbo, binti huyo wa miaka 13 "alijua kuwa ni mja mzito, na alijua maana yake, lakini sio kabisa", aliongeza.
Dkt Datar anasema kuwa ameshauri mimba hiyo itolewe kwa sababu ya kimatibabu.
Ukubwa wa ubakaji, India
Mtoto mmoja wa chini ya miaka 16 anabakwa kila dakika 155, mtoto wa chini ya miaka 10 kila masaa 13.
Zaidi ya watoto 10,000 walibakwa mwaka 2015.
Wanawake milioni 240 wanaoishi nchini India waliolewa kabla ya kufikisha miaka 18.
Asilimia 53.22% ya watoto ambao wanashiriki masomo ya serikali, wamepitia aina moja au nyingine ya bughudha ya kimapenzi.
Asilimia 50% ya wahusika wa dhulma za ngono wanafahamika kwa mtoto mhasiriwa "watu wanaoaminika au walezi wao"