Gavana Nigeria aunda wizara ya furaha na kutoshelezwa kwa wanandoa

Gavana Okorocha amemteua dadake kuongoza wizara hiyo mpya

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Gavana Okorocha amemteua dadake kuongoza wizara hiyo mpya
Muda wa kusoma: Dakika 1

Gavana wa jimbo moja kusini mashariki mwa Nigeria ameunda wizara mpya ya furaha na kutoshelezwa kwa wanandoa na akamteua dada yake kuwa kamishna wa wizara hiyo.

Uteuzi huo umefanywa na gavana wa jimbo la Imo Rochas Okorocha wiki chache tu baada yake kushutumiwa vikali kwa kuweka sanamu za kiongozi wa Afrika Kusini Jacob Zuma na viongozi wengine wanaokumbwa na utata katika maeneo mbalimbali jimboni humo.

Mwandishi wetu jijini Abuja Chris Ewokor anasema raia wa Nigeria kwenye mitandao ya kijamii wamekuwa wakizungumzia uteuzi huo ambao si wa kawaida.

Baadhi wanautazama kama "mzaha ambao umezidi" katika utawala nchini Nigeria.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Gavana Rochas Okorocha ameendelea kushutumiwa kutokana na hatua yake ya kuweka sanamu za watu mashuhuri maeneo mbalimbali jimbo lake.

Hii ni mara ya kwanza kwa jimbo lolote lile kuwa na wizara ya furaha na kutoshelezwa kwa wanandoa.

Kamishna mpya Bi Ogechi Ololo ambaye ni dadake gavana huyo kabla ya uteuzi wake alikuwa naibu mkuu wa watumishi wa gavana aliyeangazia masuala ya ndani na ya kimataifa.

Kufikia sasa, bado haijabainika majukumu yake yatakuwa ni yapi kama kamishna wa wizara ya furaha na kutoshelezwa kwa wanandoa.