Wanawake nchini Iran wazuiwa kuhudhuria mechi kati ya Iran na Syria

Chanzo cha picha, EPA
Wanawake nchini Iran walizuiwa kuingia uwanja wa kitaifa ambapo timu ya taifa ya nchi hiyo ilikuwa ikicheza mechi ya kufuzu kombe la dunian dhidi ya Syria licha ya wao kuwa na tiketi.
Wanawake hao walikusanyika nje ya uwanja wa Azadi mjini Tehran kulalamika wakati waliamrishwa kuondoka, huku wanawake raia Syria wakiruhusiwa kuingia uwanjani bila tatizo lolote baada ya kuonyesha paspoti zao.
Wanawake wamepigwa marufuku ya kuhudhuria mechi za kandanda ya wanaume nchini Iran.
Wanawake kadha walikuwa wamenunua tiketi kwa njia ya mtandao wiki moja mapema kabla ya mechi.

Chanzo cha picha, AFP/Getty Images
Lakini shiriko la kandanda nchini Iran lilisema kuwa tiketi hizo ziliuzwa kimakosa na kuahidi kuwarejeshea pesa wanawake ambao walikuwa tayari wamezinunua.
Wale waliokuwa na tiketi hata hivyo waliamua kuelekea uwanjani jana Jumanne wakitaka kujaribu ikiwa wangeruhusiwa kuingia.
"Hawakuturuhusu kuingia, walitupiga picha na kuchukua video na kutishia kutukamata. Kisha wakakusanya tiketi zetu na kuzichukua. shabiki mmoja alianiska katika mtandao wa twitter.

Chanzo cha picha, AFP/Getty Images








