Je wamkumbuka vipi mcheza soka El Hadji Diouf?

El Hadji Diouf
Maelezo ya picha, Je wamkumbuka vipi mchezaji El Hadji Diouf?

Wakati ya kipindi cha taaluma yake ya usakataji soka, El Hadji Diouf alipata sifa ya kijana mtukutu wa kandanda.

Sasas akiwa amestaafu, mchezaji huyo wa kimataifa wa Senegal anasema kuwa sifa ya kijana mtukutu wa kandanda haukuwa hakuwa nzuri.

El Hadji Diouf ni shujaa nchini Senegal na kila mahala anakokwenda hushangiliwa na mashabiki wakiwemo vijana na hata wazee.

Watu nchini Senegal bado wanamshukuru kwa wajibu aliotekeleza wakati wa kombe la dunia mwaka 2002 nchini Japan na Korea Kusini.

Lakini nchini Uingereza anakumbukwa kwa sarakasi zake uwanjani kuliko umahiri aliokuwa nao katika usakataji kandanda.

Ni tabia ililomfuata hadi kwa ligi za Uingereza alipocheza na Liverpool na Blackburn Rovers hadi Bolton Wanderes na Rangers ya Scotland.

Senegalese defender Khalilou Fadiga (R) celebrates his goal from a penalty kick with teammates Henri Camara (L-#7) and El Hadj Diouf (C) in their Group A match against Uruguay at the 2002 FIFA World Cup Korea/Japan in Suwon, 11 June 2002.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kombe la dunia mwaka 2002 El Hadj Diouf (kati kati)

Diouf aliwatemea mate wapinzani na kuwakabili wasimamizi wa mechi na wapinzani.

Lakini sasa akiwa amestaafu anaeleza historia.

Mimi ni simba, nina tabia hiyo na ninataka watu wanisheshimu.

Diouf ambaye sasa amehamia mji mkuu wa Senegal Dakar, anasema kwa mara kadha hakueleweka vyema wakati wa siku zake akicheza England.

Hata hivyo anakiri amefanya mambo mabaya.

Alipoulizwa na mambo yapi, alisema alikuwa akiwatemea mate wapinzani labda walipomuambia kitu ambacho hakukipenda.

El Hadji Diouf and President Macky Sall

Chanzo cha picha, El Hadji Diouf

Maelezo ya picha, Rais Macky Sall na El Hadji Diouf