Maelezo ya picha, Fionn, Luna na Roby wakiwa kituoni wamiliki wao walipoenda kupiga kura Cumbria
Wapiga kura walipokuwa wanafika vituoni kupiga kura Uingereza, mbwa wa kila aina hawakuachwa nyuma.
Na punde si punde, watu walianza kugundua kwamba wanyama hao walikuwa wengi sana ajabu, na kitambulisha mada cha #DogsAtPollingstations (Mbwa vituo vya kupigia kura) kikaanza kuvuma mitandaoni.
Kando na mbwa, kunao watoto, paka na hata nungunugu walionekana na kuvutia watu vituoni.
Chanzo cha picha, Twitter/@SAMiCURE
Maelezo ya picha, Phoebe alisubiri nje ya kituo cha kura Manchester
Wengi walipakia picha za mbwa wao mtandaoni Alhamisi asubuhi na katika kipindi cha saa mbili za kwanza baada ya vituo kufunguliwa, ujumbe 8000 kuhusu mbwa ulikuwa umepakiwa mtandaoni.
Mtindo kama huo ulionekana katika uchaguzi wa mitaa mwezi uliopita, kura ya maoni kuhusu kujiondoa kwa Uingereza kutoka Umoja wa Ulaya na wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka jana.
Mwaka huu, Twitter hata walitoa kibonzo cha mbwa akiwa amevalishwa bendera ya Uingereza.
Twitter walishirikiana na wakfu wa The Dogs Trust kutetea kuwepo kwa mazingira bora ya mbwa kwenye vituo vya kupigia kura.
Chanzo cha picha, Twitter/@DachshundOtto
Maelezo ya picha, Otto na Ava wavumilia kibaridi kikali asubuhi katika kituo cha kupigia kura Hampshire
Chanzo cha picha, Twitter/@TheSpeer7
Maelezo ya picha, Max akiwa Tamworth, Staffordshire alionekana kutatizwa na upweke kiasi
Chanzo cha picha, Twitter/@Thefpl_vet
Maelezo ya picha, Si mbwa pekee waliofika vituoni kwa njia ya kipekee. Hapa mbwa Finlay & Ivy wanasubiri nje ya kituo cha polisi wakiwa na watoto wawili, Lexi wa miaka miwili na Owen wa mwaka mmoja katika kituo cha kupigia kura cha shule ya msingi ya Whinstone, Ingleby Barwick.
Chanzo cha picha, Peter Maude
Maelezo ya picha, Skye alihakikisha kwamba mpiga picha anapata picha yake nzuri eneo la Essex
Chanzo cha picha, Twitter/@falcoretweets
Maelezo ya picha, Lakini Hugo aliyekuwepo kituoni Nottingham alionekana kutatizwa na mwasho...
There was an interruption when an unexpected guinea pig popped up.
Maelezo ya picha, Nungubandia buyu kwa jina Sergeant Pepper, anayefahamika pia kama 'The Wig' alihakikisha nungubandia pia hawaachwi nje.
Lakini mbwa bado walikuwa ndio wengi.
Chanzo cha picha, Deli
Maelezo ya picha, Deli wa aina ya dachshund akiwa London magharibi alihakikisha anamwacha mmiliki wake apige kura kwa faragha
Chanzo cha picha, Twitter/@jodiedoubleday
Maelezo ya picha, Two-year-old Romanian rescue Marlowe wa asili ya Romania na mwenye miaka miwili alikuwa kituoni Canterbury, Kent
Chanzo cha picha, Twitter/@DrRJWalker
Maelezo ya picha, Digby almaarufu Mr Woofs alifika Leicester kutekeleza majukumu yake mbele ya umma kwa kuwa nadhifu na 'mstaarabu'
Chanzo cha picha, Georgie
Maelezo ya picha, Mtazame hapa Bruce wa aina ya Dalmatian aliyesubiri mmiliki wake kwa hamu Derbyshire
Chanzo cha picha, Twitter/@pedventurelurcher
Maelezo ya picha, Ped mbwa wa aina ya Lurcher alionekana kuangazia zaidi kucheza na kujigaragaza juu ya nyasi Surrey.
Chanzo cha picha, Twitter/@H_Ingram
Maelezo ya picha, "Mbona mwaingia huko?" anaonekana kushangaa Mavis akiwa Bury, Lancashire
Baadhi ya mbwa aina ya Pooch hawakuweza kufika vituoni, lakini wanaonekana kutotaka kuachwa nje:
Chanzo cha picha, Twitter/@Mansehound
Maelezo ya picha, Wamiliki wa Sirius The Dog eneo la Knockbain, Scotland walipiga kura yao mapema kupitia posta. Lakini hawakutana kuachwa nje katika kusambaza picha za mbwa
Kuliwepo hata hivyo na wanapaka, na kitambulisha mada ya #catsatpollingstations (paka vituoni) pia kilivuma kiasi.
Chanzo cha picha, Twitter/ @cbowyercreative
Maelezo ya picha, Paka hutu alionekana Clare Bowyer eneo la Colburn, North Yorkshire. Hakukuwepo na mbwa karibu.
Hata nungunungu huyu kwa jina Friday alitaka kushiriki Hemel Hempstead.
Chanzo cha picha, Toni Lambert
Maelezo ya picha, Nungunungu kwa jina Friday katika kituo cha kura Hemel Hempstead
Na farasi je? Walikuwepo pia.
Chanzo cha picha, Twitter/@FontwellPark
Maelezo ya picha, Sunset Skye akiwa Sussex Magharibi
Chanzo cha picha, Twitter/ @kazzimazzi
Maelezo ya picha, Na mwisho kabisa kulikuwa na kondoo na mwanakondoo wake kituo cha kura cha Melness, Sutherland.