Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Maneno ya Kiswahili yaongezwa kamusi ya Kiingereza Kenya
Maneno kadha ya Kiswahili yameongezwa kwenye kamusi ya Kiingereza ambayo inakusudiwa kutumiwa na wanafunzi wa shule za msingi nchini Kenya.
Kamusi hiyo imechapishwa na matbaa ya Chuo Kikuu cha Oxford (OUP), na ni makala ya tatu.
Pia, kuna maneno yenye asili ya lugha nyingine za Afrika Mashariki au yaliyotoholewa na kuanza kutumiwa katika Kiswahili, ambayo yameongezwa kwenye kamusi hiyo.
Miongoni mwa maneno hayo ni:
•Bodaboda - Baiskeli au pikipiki inayotumiwa kwa uchukuzi wa abiria
•Mwananchi - Kwa maana ya mtu wa kawaida au raia wa kawaida
•Daladala - (nchini Tanzania) mabasi madogo yanayotumiwa kwa uchukuzi wa abiria
•Sambaza - Kugawa au kueneza kitu muhimu au cha thamani kwa watu wengine
•Mwalimu - Neno linalotumiwa kabla ya kutaja jina la mtu anayeheshimika au anayeenziwa, ambaye anaweza kutoa ushauri au ujuzi kwa wengine. Mfano, Mwalimu Nyerere.
Maneno ya Kiswahili ambayo yamewahi kuingizwa kwenye kamusi za Kiingereza ni pamoja na Shamba na Safari.