Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
EAC yaidhinisha kiswahili kuwa lugha rasmi
Bunge la Afrika Mashariki limepitisha azimio la kuifanya lugha ya kiswahili kuwa lugha rasmi ya jamii ya Afrika Mashariki kulingana na gazeti la The Citizen nchini Tanzania.
Gazeti hilo linasema kuwa wajumbe wa bunge hilo wamekubaliana kwamba mabadiliko hayo yalikuwa yakisubiriwa sana kwa kuwa lugha hiyo imechukua jukumu kubwa la kuwaunganisha wakaazi wa Afrika Mashariki.
Hatua inayofuata ni kwamba mkataba wa EAC utalazimika kufanyiwa marekebisho .