Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Lugha yamkwamisha mtalii wa Kichina nchini Ujerumani
Safari ya mtalii mmoja kutoka nchini China aliyeenda kutalii Ulaya imeishia kwenye moja ya kambi za kuhifadhia wakimbizi nchini Ujerumani baada ya kuomba usaidizi kutoka kwa mamlaka nchini humo.
Mtalii huyo alipoteza pochi akiwa likizo mjini Heidelberg na alipotoa taarifa polisi alishindwa kueleweka kutokana na ugumu wa lugha.Badala yake akatakiwa kujaza fomu za kuomba hifadhi kwa siku 12 kwenye kambi ya wakimbizi iliyopo mamia ya kilomita kutoka mjini.
Mkanganyiko ulimalizwa na mfanyakazi mmoja wa shirika la misaada,programu ya kutafsiri ya Kichina na baadhi ya watalii waliokuwa wakielekea nchini Italia kwa mapumziko.