Atengeza kitabu cha Quran cha mita 700 kwa mkono Misri

Chanzo cha picha, Reuters
Raia mmoja wa Misri aliyewacha shule anatumai kuweka historia baada ya kutumia muda wa miaka mitatu akitengeza kile kinachoonekana huenda ikawa Quran kubwa zaidi duniani.
Quran hiyo inayotengezwa na Saad Mohammed ambayo ameipamba, ina urefu wa mita 700 ikimaanisha kwamba inapofunguliwa ina urefu wa mita 381 sawa na jumba la Empire State.
Na kufikia sasa bwana Mohammed anayeishi katika mji wa Belqina kaskazini mwa Cairo amefadhili kila sentimita ya mradi wake.
Lakini ana matumaini makubwa .

Chanzo cha picha, Reuters

Chanzo cha picha, Reuters
Anaamini kwamba kitabu hicho ni kirefu mno kuvunja rekodi za Guiness World Records ambapo hakuna rekodi iliowekwa ya Quran ndefu zaidi ilioandikwa kwa mkono.
Lakini ili kiafikia ndoto yake na kufanikiwa katika vitabu hiyo vya rekodi za Guiness anataka usaidizi wa gharama ya kuingia katika shindano hilo.
''Quran hii ina urefu wa mita 700 na kwa kweli hiyo ni karatasi kubwa sana'', aliambia runinga ya Reuters.
''Nimejidhamini mwenyewe na mimi ni mtu wa mapato ya kawaida.Sina mali ama chochote kile''.

Chanzo cha picha, Reuters

Chanzo cha picha, Reuters

Chanzo cha picha, Reuters












