Ibrahimovic apigwa marufuku mechi tatu

Zlatan Ibrahimovic na Tyrone Mings hawakuadhibiwa

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Zlatan Ibrahimovic na Tyrone Mings hawakuadhibiwa

Mshambuliaji wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic, amapigwa marufu ya mechi tatu, baada ya kumchezea vibaya mchezaji wa Bournemouth Tyrone Mings, walipotoka sare ya 1-1 siku ya Jumamosi.

Hii inafuatia kisa kilichotoea mnamo dakika ya 44. Kisa hicho hakikutambuliwa na maafisa wa mechi lakini kilinaswa kwenye video.

Mfungaji huyu bora wa Manchester, sasa atakosa mechi kati ya Man U na Chelsea na pia Middlesbrough na West Brom.

Hata hivyo atacheza mechi ya nyumbani na Everton tarehe 4 mwezi Aprili.