Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Rais mpya wa Somalia Mohamed Farmajo akabidhiwa mamlaka
Aliyekuwa rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud amemkabidhi mamlaka rais mpya aliyechaguliwa Mohamed Abdullahi Farmajo.
Rais huyo mpya alichaguliwa chini ya usalama mkali uliowekwa katika uwanja wa ndege uliopo mji mkuu wa Mogadishu kutokana na hofu ya shambulio la al-Shabab.
Farmajo alimshinda Mohamed ambaye alitaraji kwamba wabunge wangemchagua kwa awamu ya pili.
Mwandishi wa BBC Ibrahim Aden ametuma picha za aliyekuwa rais wa taifa hilo akimuonyesha mshindi wa uchaguzi huo Mohamed Farmajo baadhi ya vitu atakavyomiliki.
Kitu kilichobainika ni idadi ya zawadi kutoka kwa mataifa ya kigeni.
Ikulu ya rais nchini humo imepokea zawadi kutoka kwa mashirika ya Umoja wa Ulaya hadi miungano ya vyuo vikuu vya Arabuni.