Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Marais wa zamani waungana na Farmajo Somalia
Picha ya waliokuwa marais wa zamani nchini Somalia wakishikana mikono na rais mpya Mohamed Abdullahi Farmajo imesambazwa mara nyingi katika mitandao ya kijamii na kupongezwa kwa umoja huo.
Hassan Sheikh Mohamud na Sharif Sheikh Ahmed walipoteza kwa Mohamed katika uchaguzi ulioshirikisha wagombea wengine 20.
Taifa la Somalia limebadilisha marais mara 12 tangu 1960 na limekuwa na mapinduzi pamoja na mauaji ya kiongozi.
Ushindi wa Mohamed umeendeleza utamaduni wa miaka mingi wa Somalia kutochagua rais aliyepo madarakani.
Bw Mohamud alikuwa rais 2012 na alitumai kuchaguliwa kwa awamu ya pili lakini wabunge walimchagua Mohamed katika uchaguzi wa siku ya Jumatano.
Sheikh Ahmed alikuwa rais wa Somalia kutoka 2009 hadi Mohamud alipomshinda 2012.