Rais mpya wa Somalia Mohamed Farmajo akabidhiwa mamlaka

Rais mpya wa Somalia Mohamed Farmajo akabidhiwa mamlaka
Maelezo ya picha, Rais mpya wa Somalia Mohamed Farmajo akabidhiwa mamlaka

Aliyekuwa rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud amemkabidhi mamlaka rais mpya aliyechaguliwa Mohamed Abdullahi Farmajo.

Rais huyo mpya alichaguliwa chini ya usalama mkali uliowekwa katika uwanja wa ndege uliopo mji mkuu wa Mogadishu kutokana na hofu ya shambulio la al-Shabab.

Farmajo alimshinda Mohamed ambaye alitaraji kwamba wabunge wangemchagua kwa awamu ya pili.

Rais Farmajo akabidhiwa mamlaka nchini Somalia

Chanzo cha picha, Twitter

Maelezo ya picha, Rais Farmajo akabidhiwa mamlaka nchini Somalia

Mwandishi wa BBC Ibrahim Aden ametuma picha za aliyekuwa rais wa taifa hilo akimuonyesha mshindi wa uchaguzi huo Mohamed Farmajo baadhi ya vitu atakavyomiliki.

Kitu kilichobainika ni idadi ya zawadi kutoka kwa mataifa ya kigeni.

Rais wa zamani wa Somalia kushoto baada ya kumakabidhi rais mpya kulia mamlaka
Maelezo ya picha, Rais wa zamani wa Somalia kushoto baada ya kumakabidhi rais mpya kulia mamlaka

Ikulu ya rais nchini humo imepokea zawadi kutoka kwa mashirika ya Umoja wa Ulaya hadi miungano ya vyuo vikuu vya Arabuni.