Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mahakama kuamua kuhusu mpaka wa Kenya na Somalia
Mahakama ya kimataifa kuhusu haki, leo itatoa uamuzi wake wa iwapo ina uwezo wa kusikiliza kesi kuhusu mzozo wa mpaka wa baharini kati ya Kenya na Somalia.
Mataifa hayo mawili yanazozania eneo moja ndani ya bahari hindi linalodaiwa kuwa na utajiri mkubwa wa hifadhi ya mafuta na gesi .
Somalia inataka mpaka huo kupanuliwa kuelekea kusini, lakini Kenya inasema kuwa mataifa hayo mawili yalitia saini makubaliano ya swala hilo mwaka 2009 na hivyobasi hakuna umuhimu wa mahakama hiyo kuingilia kati.
Lakini bunge la Somalia limepuuzilia mbali makubaliano hayo