Jengo kubwa laporomoka Iran na kuua wengi

Hakuna kilichobaki wakati jengo hilo la ghorofa 17 lilipoporomoka

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Hakuna kilichobaki wakati jengo hilo la ghorofa 17 lilipoporomoka

Wazima moto wengi wanahofiwa kuaga dunia baada ya jengo moja kubwa kwenye mji mkuu wa Iran Tehran, kushika moto na kuporomoka.

Wazima moto 200 walikabiliana na moto huo kwenye jengo hilo la ghorofa 17 kwa saa kadha, kabla ya kuporomoka kwa sekunde chache.

Zaidi ya watu 200 pia nao waliripotiwa kujeruhiwa kwenye mkasa huo.

Jengo hilo ambalo ujenzi wake ulikamilika mwaka 1962, lilikuwa wakati mmoja jengo refu zaidi mjini Tehran.

Moto huo unaripotiwa kuanza mwendo wa saa 04:30 GMT siku ya Alhamisi, wakati watu hawakuwa bado wameingia.

Wazima moto walikuwa wamepambana na moto huo kwa saa kadha

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Wazima moto walikuwa wamepambana na moto huo kwa saa kadha

Magari kumi ya kuzima moto yalifika eneo hilo na vituo vya runinga viliripoti kuwa wazima moto kadha walikuwa ndani ya jengo wakati liliporomoka.

Kituo kimoja cha runinga cha serikali kilinukuu afisa mmoja akisema kuwa kati ya watu 50 na 100 wanaaminiwa kukwama chini ya vifusi.

Jengo hilo lilikuwa ghorofa la kwanza refu mjini Tehran

Chanzo cha picha, TASNIM NEWS AGENCY/REUTERS

Maelezo ya picha, Jengo hilo lilikuwa ghorofa la kwanza refu mjini Tehran
Waokoaji walifanikiwa kuwaokoa baadhi ya wazima moto

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Waokoaji walifanikiwa kuwaokoa baadhi ya wazima moto
Baadhi ya wale waliosurika waliangua kilio

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Baadhi ya wale waliosurika waliangua kilio