Bunge la Uturuki lajadili kuongeza mamlaka ya Rais

Rais wa Uturuki Recep Tayyip amekuwa madarakani tokea mwaka 2002
Maelezo ya picha, Rais wa Uturuki Recep Tayyip amekuwa madarakani tokea mwaka 2002

Bunge la nchi ya Uturuki limetoa idhini ya awali kwa katiba mpya itayoimarisha kwa kiasi kikubwa mamlaka ya Rais.

Makala za mwisho zilipitishwa Jumapili iliyopita, chini ya uongozi wa chama cha AK walipata tatu ya hamsini ya kura nyingi zinaohitajika.

Kutakuwa na awamu ya pili ya upigaji kura baadae wiki hii.

Rais Recep Tayyip Erdogan amesema mabadiliko yataiweka Uturuki katika mstari na nchi kama Ufaransa na Marekani.

Wapinzani wanasema ni sawa na kuchukua madaraka kwa nguvu na kwamba kama katiba hiyo mpya itapitishwa na bunge kura za maoni zitapigwa.