Argentina hoi kwa Brazil yachapwa 3-0

Brazil

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha, Washambuliaji wa Brazil wakishangilia kwa staili ya kupiga simu

Michezo mitano ya kuwania tiketi ya kufuzu kwa fainali za kombe la mwaka 2018, imecheza kwa ukanda wa Marekani Kusini.

Brazil wakicheza katika dimba la Belo Horizonte, wamewachapa Argentina kwa mabao 3-0, mabao ya brazili yakifungwa na Philipe Couthino, Neymer, na Paulinho.

Venezuela wakicheza nyumbani nao wameibuka na ushindi wa kishindo kwa kuwachapa bolivia kwa mabao 5-0.

Paraguay wamekubali kichapo nyumbani baada ya kufungwa mabao 4-1 na Peru,Uruguay wakashinda kwa mabao 2 - 1 dhidi ya Ecuador

Uruguay

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha, Mfungaji wa bao la kwanza la Uruguay Sebastian Coates akishangilia na Diego Godín

Colombia wakashindwa kuutumia vyema uwanja wa nyumbani baada ya kutoshana nguvu na Chile kwa sare ya bila kufungana.