Pakistan na India zashambuliana

Kila upande umesema umechukua hatua kulipiza kujibu mashambulio hayo.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Kila upande umesema umechukua hatua kulipiza kujibu mashambulio hayo.

Pakistan na India zimelaumiana kwamba zimefanya mashambulio katika mpaka baina yao kwenye eneo la Kashmir.

Kila upande umesema umechukua hatua kulipiza kujibu mashambulio hayo.

Hakuna aliyesema kama kumetokea maafa yoyote.

Juma hili India ilifanya operesheni iliyolengwa maeneo ya wapiganaji, upande wa Pakistan.

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha, Juma hili India ilifanya operesheni iliyolengwa maeneo ya wapiganaji, upande wa Pakistan.

Jeshi la Pakistan limesema wanajeshi wa India, walifyatua risasi na mizinga karibu na mji wa Bhimber.

Huku nyuma, Shirika la habari la India, Press Trust of India, limearifu kuwa baadhi ya wana kijiji upande wa India, mashariki kidogo, wamehamishwa, kwa sababu ya risasi nyingi zinazofyatuliwa na Pakistan.

Awali juma hili, India ilisema ilifanya ile iliyoita operesheni iliyolengwa dhidi ya maeneo ya wapiganaji, upande wa Pakistan.