Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Pakistan na India zashambuliana
Pakistan na India zimelaumiana kwamba zimefanya mashambulio katika mpaka baina yao kwenye eneo la Kashmir.
Kila upande umesema umechukua hatua kulipiza kujibu mashambulio hayo.
Hakuna aliyesema kama kumetokea maafa yoyote.
Jeshi la Pakistan limesema wanajeshi wa India, walifyatua risasi na mizinga karibu na mji wa Bhimber.
Huku nyuma, Shirika la habari la India, Press Trust of India, limearifu kuwa baadhi ya wana kijiji upande wa India, mashariki kidogo, wamehamishwa, kwa sababu ya risasi nyingi zinazofyatuliwa na Pakistan.
Awali juma hili, India ilisema ilifanya ile iliyoita operesheni iliyolengwa dhidi ya maeneo ya wapiganaji, upande wa Pakistan.