Moto wa kiwanda wawaua watu 20 Bangladesh

Moto huo ulisambaa kwa haraka katika nyumba hiyo ya ghorofa nne

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Moto huo ulisambaa kwa haraka katika nyumba hiyo ya ghorofa nne

Watu ishirini wameuwawa nchini Bangladesh katika moto mkubwa katika kiwanda kimoja, uliosababishwa na mlipuko wa kifaa cha kuchemsha maji.

Zaidi ya watu 70 wamejeruhiwa viungani mwa mji mkuu Dhaka, na inaarifiwa kwamba huenda idadi ya walioaga ikaongezeka.

Polisi wanasema kwamba zaidi ya watu 100 walikuwa wakifanya kazi katika kiwanda hicho, na kwamba moto huo ulisambaa kwa kasi katika jengo hilo la ghorofa nne.

Wazima moto wakiwabeba waathiriwa kwenye ajali hiyo ya moto

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Wazima moto wakiwabeba waathiriwa kwenye ajali hiyo ya moto