Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Moto wa kiwanda wawaua watu 20 Bangladesh
Watu ishirini wameuwawa nchini Bangladesh katika moto mkubwa katika kiwanda kimoja, uliosababishwa na mlipuko wa kifaa cha kuchemsha maji.
Zaidi ya watu 70 wamejeruhiwa viungani mwa mji mkuu Dhaka, na inaarifiwa kwamba huenda idadi ya walioaga ikaongezeka.
Polisi wanasema kwamba zaidi ya watu 100 walikuwa wakifanya kazi katika kiwanda hicho, na kwamba moto huo ulisambaa kwa kasi katika jengo hilo la ghorofa nne.