Ufilipino ni ‘ruksa kufanya ngono na mtoto mwenye miaka 12’

Watoto wenye umri wa miaka 12 ambao ndio kwanza wanaingia kipindi cha kubalehe, wakati ambapo hawana ueleo wowote kuhusu mahusiano ya kingono.

Kwa miongo kadhaa raia wa Ufilipino wamekuwa wakifanya ngono kihalali na watoto wenye umri huo.

Taifa hili la kusini mwa Asia ni miongoni mwa mataifa machache duniani ambayo yameweka ruhusa ya kukutana kimwili duniani kwa kiwango kidogo, ingawa utofauti huu unachanganya kutokana na kuwa na utofauti wa sheria kwa kila taifa.

Wataalamu wanasema kuwa idhini katika masuala ya kujamiiana iko chini nchini Ufilipino ambapo afya za watoto zinakuwa hatarini na pia kuchangia ongezeko la unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto.

Sheria tata ambayo bado inatumika mpaka leo tangu mwaka 1930, inafanya suala la ubakaji kushindwa kupata ufafanuzi wa kutofautisha upi ni ubakaji na upi sio ubakaji ; na kufanya watuhumiwa wa ubakaji kushindwa kuhukumiwa kisheria.

Hata hivyo mambo yatabadilika sana hivi karibuni.

Mwishoni mwa mwaka 2020, bunge la Philippine, baada ya kampeni zilizochukua miongo kadhaa kutoka kwa taasisi mbalimbali kutetea haki za watoto , na wengi wakitaka umri wa mtu kuanza mahusiano ya kingono kuwa miaka 16 kisheria.

Bado mapendekezo hayo hayajapitishwa na Rais Rodrigo Duterte kuwa sheria. Ni hatua ambayo inaleta matumaini kwa wengi kuwa unyanyasaji wa watoto utafikia mwisho wake baada changamoto za miongo kadhaa.

Chanzo cha Utamaduni huo

Katika dunia hii, umri wa idhini ya kuruhusiwa kuanza kujihusisha kingono ukiwa ni kati ya miaka 11 hadi 18, kuna baadhi ya mataifa ambayo bado wanaruhu chini ya miaka 14 au 15.

Mataifa mengi ya Amerika ya Kusini na Asia, na suala la kesi ya Ufilipino, wamekuwa wakihalalisha utaratibu huo kwa kuegemea kwenye masuala ya sheria za dini na utamaduni pamoja na sheria ambayo ilikuepo tangu enzi za ukoloni wa utawala wa Uhispania ambao uliisha mwaka 1898.

Sheria ya Ufilipino tangu enzi za ukoloni pamoja na mitazamo ya kidini inchangia katika uendelezaji wa utamaduni huo.

"Wakati nchini Ufilipino umri wa kujihusisha na masuala ya ngono ni kuanzia miaka 12 tangu mwaka 1930s, bado tunatumia sheria ambayo tumerithi utawala kutoka kwa utawala wa kikoloni ambao uliwekwa karne tatu zilizopita pamoja na utamaduni wote," alifafanua Dkt. Bernadette ambaye ni mkurugenzi wa umoja wa kutetea haki ya mtoto, katika chuo kikuu cha Manila, nchini Ufilipino.

Mpaka mwaka 2015, umri wa kuruhusu kujamiiana nchini Uhispania ni kuanzia miaka 13,ni miongoni mwa nchi chache barani ulaya zenye sheria ya namna hiyo ingawa kwa sasa wameweka mpaka kuanzia miaka 16.

Mtazamo wa kisaikolojia na kimwili

"Sheria ya ubakaji ambayo inahusisha uhalifu wa kati ya mtu mzima na mtoto ambaye umri wake umetajwa kisheria.

Katika umri fulani, mtoto mdogo hawezi kukubaliwa kufanya ngono kwa sababu hajafikia umri wa kufanya maamuzi juu yake," anafafanua. Patrizia Benvenuti, mkurugenzi wa Ulinzi wa Mtoto kutoka shirika la kimataifa ia watoto la Unicef nchini Ufilipino.

Hivyo basi katika taifa hilo mtu yeyote anayefanya ngono na mtoto ambaye yupo chini ya miaka 12 ndio anapatikana na hatia kwa mujibu wa sheria.

Kwa miongo kadhaa, taasisi mbalimbali zimefanya kampeni nyingi kulinda usalama wa watoto Ufilipino.

"Hili ni tatizo kubwa .Akili ya mtu inapevuka mpaka anapofika miaka 25. Kuna ushaidi wa kutosha kuhusu hili.

Kuna wale ambao wanasema ni sawa kwa mtoto mwenye miaka 12 ni sawa kuingia kwenye masuala ya ngono kwa utafiti wa kisayansi juu ya ukuaji wa ubongo, na ukuaji wa kihisia ",aliongeza mtaalamu.

"Mtoto wa miaka 12 , ni rahisi kupata maambukizi ya maagonjwa yanayosababishwa na kuhusiana kingono na hata kansa ya kizazi.Ujauzito katika umri huo unamuweka mtoto na mama katika hali ya hatari, aliongeza", Madrid adds.

Wataalamu wote wanasema, ni rahisi sana watoto wenye umri huo kurubuniwa na watu wazima .

Uharaka wa kupitisha sheria hiyo

Benevenuti anasema kupitishwa kwa sheria hiyo ni mhimu kwasababu itaweza kuwalinda watoto katika mahusiano na watu wazima ambao wanawarubuni ili kufanya nao ngono .

Na hii kupelekea watoto hao kukatisha masomo wakiwa na umri mdogo kwasababu ya ujauzito na kuapata mimba zisizotarajiwa na kupata magonjwa.

Nchini Ufilipino, mtoto mmoja kati ya watoto watano, walio kati ya umri wa miaka 13 na 17 amekumbwa na unyanyasaji wa na tatizo hili linawaathiri watoto wote wa kiume na wa kike, kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na UNICEF mwaka 2015.

Ndio maana penekezo pia lilijumuisha ulinzi sawa kwa wote wavulana na wasichana katika visa vya ubakaji, jambo ambalo halijajumuishwa katika sheria ya sasa.

Ufilipino pia ni miongoni mwa nchi zenye idadi kubwa ya uzalishaji na usambazaji wa filamu na picha za ponografia za watoto.

Unicef inakadiria kuwa umri unaotambulika kisheria wa mtu kubakwa ni sababu ya kimsingi ya viwango hivi vya unyanyasaji wa kingono.

Kubadilika kimawazo

Wafilipino wengi , sawa na like Madrid, walitarajia mageuzi yapitishwe haraka katika Seneti baada ya kuidhinishwa na Congress Disemba 1, 2020 kwa kura 207 na wabunge watat kupiga kura ya hapana.

"Lakini sasa inaonekana kwamba mchakato wa mageuzi hayo unazorota. Ninahofu kwamba, kama itaendelea kuchewa, mwamko wa mabadiliko hayo utazimwa na badala yake serikali itazipa kipaumbele ajenda nyingine za kisiasa ,"anasema mtaalamu .

Wanaopigia debe sheria mpya wamekuwa wakijaribu kwa miaka kadhaa kuhakikisha inajadiliwa katika Congress, lakini hilo halikufanikiwa hadi miezi michache iliyopita ambapo wabunge wa congress waliketi kujadili na kuiidhinisha.

"Kando na sheria, nchi hii inahitaji mpango madhubuti wa elimu ya ngono ."

"Baadhi ya wabunge wa congress wna miaka mabinti zao wenye umri wa miaka 12 na , kwahivyo wanahuruma ya kutosha kuelewa kwamba msichana mwenye umri wa miaka 12 hayuko tayari kufanya ngono ," alieleza Madrid.

Daktari anakiri kwamba, licha ya kwamba sheria hiyo imepigiwa debe kwa kiasi kikubwa na taasisi , kuna "walawiti " ambao wamezungumzia dhidi yake na kukosoa uamuzi huo kwa kuandika jumbe kwenye za ukosaji kwenye wavuti wa Kitengo cha ulinzi wa watoto.

"Wengi wanatuambia kuwa watoto wenye umri wa balehe wenye miaka 12 wanapasawa kuwa huru kujiamlia wenyewe kufanya ngono au kutoifanya. Licha ya sheria, nchi hii inahitaji mpango madhubuti wa elimu ya ngono , " anasema mtaalamu.