Mwanariadha wa 2 wa Ethiopia aonyesha ishara ya kupinga serikali

Chanzo cha picha, AFP
Juma moja baada mwanariadha wa Ethiopia Feyisa Lilesa, ambaye alishinda fedha katika mashindano yaliyokamilika ya mjini Rio kugonga vyombo vya habari baada ya kufanya ishara ya kupinga akitumia miakono yake alipokuwa akikamilisha mbio hizo, sasa mwanariadha mwingine wa Ethiopia amekamilisha mbio za Quebec kwa kufanya ishara kama hiyo.
Ishara hiyo hufanywa na watu wa kabila la Oromo nchini Ethiopia, ambao wametaabika kutokana na dhuluma zinazofanywa na polisi.
Mtandaoa wa twitter nchini Canada uliandika habari wakati Ebisa Ejigu, alishinda mbio kwa muda wa 2:30:40 na kufanya ishara hiyo ya kupinga kwa mikono.

Chanzo cha picha, AFP
Baada ya kufanya ishara hiyo mjini Rio, Feyisa hajarejea nchini Ethiopia akisema kuwa anahofia maisha yake au anaweza kufungwa jela.
Shirika la kupigania haki za binadamu la Amnesty International, linasema kuwa watu 97 waliuawa wakati vikosi vya usalama vilifyatua risasi kwenda kwa maandamano ya amani.
Feyisa alizaliwa eneo la Ambo huko Oromia ambalo ndilo kubwa zaidi nchini Ethiopia na ambalo limekumbwa na maandamano kwa kipindi cha miezi 26 iliyopita.








