Fahamu madhara ya kuishi anga za Juu kwa muda mrefu

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 5

Wanaanga wa NASA Sunita Williams na Butch Wilmore, ambao wamekwama kwenye Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu kwa muda wa miezi 9, hatimaye watarejea duniani.

Wanaanga hao walienda kwenye kituo cha anga za juu wakiwa kwenye chombo cha majaribio cha Boeing Starliner mnamo mwezi Juni 2024 kwa safari iliyotarajiwa kuchukua siku 8 pekee wasijue kwamba ghafla ingebadilika na kuishi muda mrefu katika anga za mbali.

Je, wanaanga hao watarudi lini na watarudi vipi?

Leo Machi 12, chombo cha SpaceX, kitaanza safari ya wanaanga wa kundi la 10 kwenda kwenye kituo cha anga za mbali kikiwa na chombo Dragon. Uzinduzi wa safari hiyo utafanyika kutoka Kituo cha Anga cha NASA cha Kennedy huko Florida.

Siku ya Alhamisi, Machi 13, chombo cha anga za juu cha Dragon kitaanza safari ya kwenda kwenye Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu - kumaanisha kwamba chombo hicho kitaunganishwa kwenye kituo cha anga za juu na timu mpya itachukua nafasi ya timu ya safari ya 9 walio kwenye kituo cha anga za juu kwa sasa.

Kisha chombo hicho kitatengana na kituo cha anga za juu na kurejea duniani kati ya Machi 16 na 19, pamoja na wanaanga wa timu ya 9, na wanaanga wawili waliokwama huko.

Mwanaanga wa NASA Nick Hague atakuwa rubani wa chombo hicho katika safari ya kurejea na akishughulikia mchakato mzima kuanzia kutoka anga za mbali hadi kutua kutua majini. Pamoja nao, Sunita Williams, Butch Wilmore na mwanaanga wa Urusi Alexander Gorbunov watarudi Duniani kutumia chombo hiki.

NASA sasa inatumia chombo cha SpaceX, kampuni binafsi ya safari za anga za juu ya Elon Musk, kuwasafirisha wanaanga kwenda na kutoka kituo cha anga za juu.

Sunita Williams ataweka rekodi nyingine atakaporejea Duniani kwa kutumia chombo cha anga za juu cha SpaceX.

Atakuwa mwanaanga wa kwanza kusafiri kwenda anga za juu kwa kutumia vyombo tofauti yaani Space Shuttle, Soyuz, Boeing Starliner, na sasa Dragon.

Soma zaidi:
.

Chanzo cha picha, X / @Space_Station

Kufeli kwa chombo cha Boeing Starliner

Williams na Wilmore walisafiri katika safari ya majaribio ya chombo cha Boeing Starliner mnamo Juni 5, 2024. Safari hii ilitakiwa kuwa ya siku nane. Lakini chombo cha Starliner cha Boeing kilipata matatizo ya kiufundi. Sehemu tano za chombo hicho ziliharibika.

Chombo hicho pia kiliishiwa na heliamu hivyobasi, kikalazimika kutegemea mafuta ya kuchoma. Kutokana na sababu hizi, kurudi kwa wanaanga wote wawili kulicheleweshwa.

Hatimaye, ilibainika kuwa chombo cha Starliner hakikufaa kwa safari ya kuwarejesha wanaanga Duniani, na wanaanga hao wawili wakalazimika kusalia kwenye Kituo cha Kimataifa cha Anga cha Juu kwa muda mrefu zaidi.

Chombo cha Boeing Starliner kilirudishwa duniani, kwa kuongozwa na kompyuta kutoka duniani.

Athari za kuishi katika anga za juu kwa muda mrefu

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Wengi walionyesha wasiwasi kuhusu ikiwa kukaa kwa miezi 9 kwenye anga za mbali ni hatari kwa wanaanga na itakuwa na athari gani kwa miili yao.

Lakini wanaanga wote wawili walisema kwamba muda huu wa kukaa ulikuwa fursa adimu kwao.

"Tutatamani kila kitu kwenye anga za juu," Sunita Williams alisema, akitoa miongozo ya ISS.

Wakati huu ambao wameketi kwa muda mrefu kwenye anga za juu, wanaanga hao wawili walifanya majaribio kadhaa ikiwa ni pamoja na kutembea katika anga za juu na majaribio ya kukuza mimea angani.

Hata hivyo, kuishi kwa muda mrefu katika anga za juu kuna uwezekano wanaanga wasiweze kutembea mara baada ya kurejea Duniani, kwani hii itakuwa mshtuko mkubwa kwa mwili uliozoea kuishi bila mvutano.

Zaidi ya hayo, kusafiri kunaweza kusababisha mifupa kuwa dhaifu, ambayo pia huathiri misuli.

Kuishi kwa muda mrefu kwenye anga za mbali huathiri misuli, ubongo na macho ya wanaanga.

Utafiti wa kina ulifanyika kuchunguza jinsi mwanaanga wa Marekani Frank Rubio alivyokaa kwa muda mrefu kwenye anga za juu kulivyoathiri mwili wake.

Alikuwa mwanaanga wa kwanza kushiriki katika jaribio la kuchunguza madhara ya kufanya mazoezi kwenye anga za juu kwa kutumia vifaa kidogo tu vya mazoezi.

Maelezo haya yatakuwa muhimu kwa misheni za anga za juu.

Kwa sababu ikiwa ujumbe wa binadamu kwenda anga za mbali ungezinduliwa kwenye Mirihi, kulingana na takwimu za sasa, inakadiriwa kwamba ingechukua takriban siku 1100 - zaidi ya miaka 3 - kufika Mirihi na kurudi.

Chombo ambacho wanaanga hao watatumia kusafiri hadi Mihiri kitakuwa kidogo zaidi kuliko Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu. Hii ina maana kwamba wanaanga wataweza tu kubeba vifaa kidogo na vyepesi kwa ajili ya mazoezi.

Athari kubwa kwa mwili ni ukosefu wa nguvu za uvutano hivyo basi, uzito wa misuli na mifupa ya mikono na miguu huanza kupungua.

Kiasi kidogo sana cha nguvu za uvutano, husababisha misuli hii kushindwa kufanya kazi na huanza kudhoofika.

Uzito wa misuli unaweza kupunguzwa kwa hadi 20% baada ya wiki mbili tu ukiwa katika anga za juu, na kwa kiasi cha 30% baada ya miezi miwili hadi sita.

Pamoja na hili, kiunzi cha mifupa na mifupa katika mwili havina utendaji sawa kama ilivyo duniani. Hii husababisha mifupa kuwa dhaifu na nguvu yake kupungua.

Katika kipindi cha miezi sita kwenye anga za juu, wanaanga hupoteza hadi asilimia 10 ya uzito wa mifupa. Kwa wanaoishi duniani, kiwango sawa na hicho ni 0.5 - 1% kwa mwaka.

Hii ndiyo sababu uwezekano wa wanaanga kuvunjika mifupa unaongeza na huchukua muda mrefu kupona.

Baada ya kurejea Duniani, inaweza kuchukua hadi miaka minne kwa mifupa katika mwili kupona kabisa.

Kwa sababu hii, wanaanga hufanya mazoezi masaa mawili na nusu kila siku wanapokuwa kwenye kituo cha anga za juu na hujitahidi kula lishe nzuri.

Kwa sababu hakuna nguvu ya mvutano kwenye anga za mbali, uti wa mgongo wa wanaanga hupanuka na kimo chao huongezeka kidogo.

Soma zaidi:

Imeafsiriwa na Asha Juma