Jinsi ya kutengeneza oksijeni kwenye mwezi

f

Chanzo cha picha, Sierra

Maelezo ya picha, Kampuni ya Sierra Space inafanya kazi kuunda kifaa cha kuzalisha oksijeni katika mwezi
    • Author, Chris Baraniuk
    • Nafasi, BBC
  • Muda wa kusoma: Dakika 3

Ndani ya tufe kubwa, wahandisi wanatazama vifaa vyao. Kifaa kama sanduku ambalo wanatumaini siku moja litatengeneza oksijeni mwezini.

"Tumejaribu kila kitu tunachoweza duniani," anasema Brant White, meneja wa programu hiyo katika kampuni binafsi ya Sierra Space. "Hatua inayofuata ni kwenda mwezini."

Jaribio la Sierra Space lilifanyika katika Kituo cha angaza za juu cha Johnson cha Nasa katika majira ya joto ya 2024. Ni teknolojia ambayo inaweza kusambaza oksijeni kwa wanaanga wanaoishi kwenye mwezi kwa siku zijazo.

Tufe kubwa la duara lilifanyiwa majaribio na Sierra Space mwezi Julai na Agosti mwaka huu.

Wanaanga hao watahitaji oksijeni kupumua lakini pia kutengeneza mafuta ya roketi kwa ajili ya vyombo vya angani ambavyo vinaweza kurushwa kutoka mwezini na kuelekea maeneo ya mbali zaidi - ikiwa ni pamoja na kwenda sayari ya Mirihi.

dc

Chanzo cha picha, Sierra

Maelezo ya picha, Chumba hiki huunda hali ya hewa kama iliopo katika mwezi

Wakazi wa mwezini wanaweza pia kuhitaji chuma na wanaweza kuvipata kwenye uso wa mwezi. Hilo linategemea ikiwa wataweza kujenga vinu vinavyoweza kuchimba rasilimali kama hizo kwa ufanisi.

"Upatikanaji wa chuma huko unaweza kuokoa mabilioni ya dola kutokana na gharama za misheni kama hizo," anasema Bw White.

Anaeleza kuwa - kupeleka oksijeni na chuma kwenye mwezi kutoka duniani - itakuwa ngumu na ya gharama kubwa.

f

Chanzo cha picha, NASA

Maelezo ya picha, Nasa inapanga kupeleka wanaanga kwenye mwezi 2027

Akieleza umuhimu wa oksijeni kwa safari za siku zijazo za mwezini, Dkt. Paul Burke kutoka chuo kikuu cha Johns Hopkins anaeleza, kwa siku, mwanaanga atahitaji kiasi cha oksijeni takribani kilo mbili au tatu, kulingana na siha na viwango vya kazi za mwanaanga huyo.

Hata hivyo, mifumo ya oksijeni katika mwezi yanaweza kuirejesha oksijeni inayopumuliwa na wanaanga ili kutumika tena. Kama hilo litawezekana, haitakuwa muhimu kuzalisha oksijeni nyingi ili kuwaweka hai wakaazi wa mwezini.

Matumizi makubwa hasa ya oksijeni yatakuwa ni katika teknolojia, anaongeza Dk Burke, wakati wa uzalishaji wa mafuta roketi, ambayo inaweza kuwezesha uchunguzi wa anga kwa ukubwa wake.

I

Chanzo cha picha, MIT and Shaan Jagani

Maelezo ya picha, Palak Patel amekuwa akitafiti njia za kupata oksijeni na chuma kutoka katika udongo wa mwezini
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Ni wazi kwamba kupatikana kwa rasilimali nyingi zaidi mwezini ni jambo bora.

Mfumo wa Sierra Space hauhitaji kuongezwa kaboni, ingawa kampuni hiyo inasema inaweza kuizalisha baada ya kila mzunguko wa oksijeni.

Pamoja na wenzake, Palak Patel, mwanafunzi wa PhD katika Taasisi ya Teknolojia ya Massachusetts, alikuja na mfumo wa majaribio, kupata oksijeni na chuma katika udongo wa mwezi.

Bi Patel anasema mashine za baadaye za kuchimba rasilimali kwenye mwezi zinaweza kuchimba chuma, titanium au lithiamu. Nyenzo hizi zinaweza kusaidia wanaanga wanaoishi kwenye mwezi kutengeneza vipuri au vifaa vya kubadilisha vyombo vya angani vilivyoharibika.

Umuhimu wa udongo wa kwenye mwezi hauishii hapo. Bi Patel anabainisha kuwa, katika majaribio yao, aliyeyusha udongo wa kwenye mwezi na kuufanya kuwa kama kigae kigumu cheusi.

Yeye na wenzake walifanya kazi ya kugeuza udongo huu kuwa matofali magumu, ambayo yanaweza kuwa muhimu kwa ajili ya kujenga majengo kwenye mwezi.

Imetafsiriwa na Rashid Abdalla na kuhaririwa na Ambia Hirsi