Ni nini hutokea kwa miili ya wanaanga wanapofariki angani?

Chanzo cha picha, NASA
Shirika la anga za juu la Marekani (NASA) linajaribu kutuma wanaanga kwenda mwezini mwaka wa 2025 na Mars katika miaka mingine kumi ijayo.
Kutuma wanadamu angani ni kazi ngumu, na vile vile ni hatari.
Takriban watu 20 wamefariki katika matukio hayo katika kipindi cha miaka 60 iliyopita.
Kati ya 1986 na 2003, watu 14 walifariki katika ajali za anga za juu za NASA.
Mnamo 1967, watatu walikufariki katika tukio la kupaa kwa chongo Apollo-1. Wengine watatu wakafariki katika safari ya Suez 11 ya 1971.
Usafiri wa anga ni mgumu na wa gharama kubwa.
Sasa safari ya anga ya kibiashara inayolipishwa pia imeanza. Usafiri wa anga unazidi kuwa jambo la kawaida.
Swali linalozuka vichwani mwa wengi ni - Je, ni nini hutokea kwa miili ya wanaanga iwapo iwatafariki baada ya kwenda angani? Je, kuna mazishi?
Unawarudishaje? Utaishia katika safari ya gharama kubwa, iliyopangwa kwa muda mrefu?
Je, iwapo wanaanga wa Marekani watafariki kwenye mwezi au katika umbali wa mamilioni ya kilomita katika siku zijazo? NASA itafanya nini? Hebu tupate majibu ya maswali haya.
Itifaki za 'NASA' zinasema nini?
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Taasisi ya Utafiti ya Utafsiri ya NASA ya Afya ya Anga huhakikisha kwamba wanaanga wana afya bora iwezekanavyo.
"Iwapo mwanaanga atafariki angani au katika 'mzunguko wa chini wa Dunia', mwili wake unaweza kurudishwa duniani ukiwa ndani ya kifaa chenye muundo wa kidonge cha capsule ndani ya saa chache," anasema Profesa Emmanuel Urquieta, anayefanya kazi katika taasisi hiyo.
Ikiwa mtu alikufariki kwenye mwezi, itakuwa vigumu kwa mwili kufika duniani kwa wakati unaotakikana. Itachukua siku chache. NASA pia imeunda itifaki ya kina ya vitu kama hivyo.
Ikiwa mtu atakufariki kwenye safari na wanaanga wanarudi Duniani kwa wakati mmoja, kipaumbele cha kwanza cha wakala ni urejeshaji salama wa wanaanga waliosalia.
Lakini, ikiwa mwanaanga atafariki njiani kuelekea kwenye obiti au mhimili (safari ya maili milioni 30), hali itakuwa tofauti.
Ikiwa kifo kitatokea kwenye Mars je, kutakuwa na mazishi?
Ni vigumu kuwarejesha wanaanga ikiwa mtu atakufa wakati anaenda mbali sana. Inaweza kuchukua miaka kurudisha mwili Duniani mwishoni mwa safari.
Hadi wakati huo, wanaanga wana jukumu la kuweka mwili katika chumba maalum au mfuko maalum wa kuhifadhi mwili.
Joto na unyevu wa kila wakati ndani ya chombo husaidia kuulinda mwili kuharibika.
Hili linawezekana katika maeneo kama vile vituo au vyombo vya angani.

Chanzo cha picha, Getty Images
Tuseme mtu afariki wakati mwanaanga anafika katika Mars.
Kwa kuwa hawatakuwa na mahali pa kuzika au kuchomea maiti, kazi itakuwa ngumu kwa wafanyakazi wenzao.
Kwa sababu kwa hilo wanapaswa kutumia nguvu nyingi. Wakati huo wanahitaji nguvu nyingi kufanya kazi iliyowapeleka.
Kumzika kwa upande mwingine, sio wazo nzuri.kwani bakteria na viumbe vingine kutoka kwa mwili vinaweza kuuchafua uso wa Mars.
Kwa hivyo mwili utawekwa kwenye begi maalum la mwili hadi utakapofika chini Duniani uweze kuzikwa au kuchomwa.














