Kipi hutokea wanaanga wanapokwama angani?

sxc

Chanzo cha picha, Getty Images

    • Author, Richard Hollingham
    • Nafasi, BBC
  • Muda wa kusoma: Dakika 4

Wanaanga wawili wa shirika la anga la Nasa la Marekani, watakaa kupita muda uliopangwa katika kituo cha anga za kimataifa. Wao sio wanaanga wa kwanza kukwama angani na huenda hawatakuwa wa mwisho.

Sunita Williams na Butch Wilmore, wako huko kwa zaidi ya miezi miwili katika misheni yao ya siku nane kwenye Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu (ISS).

ISS ndicho kituo kikubwa katika anga za juu ambacho kinatumiwa na kuendeshwa na mashirika matano ya anga za juu, ambayo ni NASA, Marekani, Roscosmos, Urusi, ESA, Ulaya, JAXA, Japan na CSA, Canada.

Inaaminika kuwa chombo cha Starliner kilichowapeleka Williams na Wilmore, kimeshindwa kuwarudisha salama duniani.

Pia unaweza kusoma
r

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wanaanga hao wawili waliondoka duniani mwezi Juni

Katika mkutano na wanahabari wa tarehe 7 Agosti, maafisa wakuu wa Nasa walielezea kwa undani lile lililotokea katika chombo hicho. Ni tatizo katika mfumo wake wa kujiendesha na baadhi ya injini zake zilijizima.

Licha ya majaribio makubwa ya chombo hicho kilipokuwa ardhini, wahandisi bado hawajaelewa tatizo hilo limesababishwa na nini. Majaribio katika obiti yanaonyesha kuwa injini hizo zinafanya kazi vizuri kwa sasa, lakini hawajajua kwanini zilizima.

Hadi wahandisi watakapokuwa na uhakika kuhusu mfumo wa uendeshaji, Williams na Wilmore wataendelea kubaki ISS. Hadi sasa bado hakuna uamuzi wa mwisho ambao umefanywa, ila huenda chombo hicho kikarudishwa duniani, bila ya wanaanga hao.

Iwapo Starliner itarejeshwa duniani bila wao, NASA inapanga kutuma chombo cha anga za juu cha SpaceX Crew Dragon chenye viti vinne na wanaanga wawili ndani yake. Ikiwa hilo litafanyika, Williams na Wilmore watalazimika kusalia kwenye kituo hicho hadi Februari 2025 na kurudi na wanaanga wa Crew Dragon.

"Kituo cha anga za juu kwa sasa kina vyumba saba vya kulala na bafu tatu," anasema mwanaanga wa Nasa, Victor Glover, ambaye alitumia miezi sita kwenye anga ya kimataifa mwaka 2020-2021.

Kuna maji ya kutosha na pia kuna chakula cha kutosha. Wanaanga ni watu waliofunzwa ambao na wamejitayarisha kwa karibu kila hali ya dharura.

"Wanaanga wanakuwa na furaha wanapokuwa huko," anasema mwanzilishi na mhariri wa tovuti ya habari za anga ya juu SpaceUpClose, Ken Kremer, "watu wengi wanafikiri wamekaa tu wako peke yao kwenye matatizo, hapana, sio hivyo."

"Sisi ni wataalamu wa kufanya safari za hatari," anasema Glover. "Tunajitahidi tuwezavyo kupunguza hatari hizo lakini kwenda angani sio kwamba hakuna hatari yoyote."

Wanakwenda kufanya nini?

zx

Chanzo cha picha, Alamy

Maelezo ya picha, Muda wa kukaa angani umeongezeka kwa sababu ya matatizo katika chombo cha Boeing's Starliner

Pamoja na kufanya majaribio ya kisayansi, wanaanga wanaokijua vyema kituo hicho na mfumo wake wa ufanyaji kazi, hutumwa kupeleka mizigo, kupeleka chakula na kufanya usafi wa vifaa.

Kwa kawaida, jasho na mkojo wa wanaanga hugeuzwa kuwa maji ya kunywa, lakini kwa sababu ya hitilafu ya hivi karibuni, wanaanga hao wanalazimika kuhifadhi mkojo, katika mazingira ambayo tayari kuna wafanyakazi wawili wa ziada.

Matukio kama haya ni adimu. Tangu Novemba 2000, kumekuwa na watu wanaoishi na kufanya kazi katika kituo

dsx

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Sergei Krikalev, akionekana hapa kwenye ISS mwaka 1998
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Mwanaanga wa Soviet Sergei Krikalev aliposafiri hadi kituo cha anga za juu cha Mir, mwezi Mei 1991, alikuwa akitarajia kukaa miezi michache huko. Wakati huo huo, nchi ambayo Krikalev alikuwa anatoka, ilianza kusambaratika.

Mwezi Agosti, vifaru vilikuwa katika mitaa ya Moscow, wafuasi wenye misimamo mikali ya kikomunisti wakijaribu kufanya mapinduzi dhidi ya kiongozi wa ki-Soviet, Mikhail Gorbachev.

"Mke wangu alikuwa akifanya kazi katika kituo cha angaza za juu cha duniani, walikuwa na wasiwasi juu yetu na tulikuwa na wasiwasi juu yao - ni wasiwasi wa pande zote," anasema Krikalev mwaka 2019.

Miezi minne baadaye, Muungano wa Kisovieti ulianguka, lakini vyombo vya kupeleka bidhaa viliendelea kupelekwa, ingawa kulikuwa na shaka kuhusu wakati gani Krikalev na mwenzake, Aleksandr Volkov, wataweza kurudi.

Kituo cha kurushia na kutua vyombo vya angaza za juu cha Soviet, kilikuwa katika nchi mpya huru ya Kazakhstan, ilimaanisha serikali ya Urusi ililazimika kuingia makubaliano kuendelea kuedesha kituo hicho.

"Nilisikia hadithi zote kwamba tumesahauliwa kwenye kituo cha juu," anasema Krikalev. "Kwa kweli haikuwa hivyo, kwa sababu kila siku tulikuwa tukiwasiliana na walio ardhini, kulikuwa na chombo ambacho kileleta kila kitu, majaribio na data na chakula na maji. Kila kitu kilikuwa kikitujia kwa ratiba."

Baada ya kuondoka Umoja wa Kisovieti, na kukaa karibu mwaka mmoja katika obiti, hatimaye alirudi katika nchi yake mpya ya Urusi na akawa miongoni mwa wafanyakazi wa kwanza kuishi kwenye kituo cha angaza za juu.

Kilicho wazi kuhusu tukio hili la sasa, ni kwamba hakuna mwenye hofu. Uamuzi wa mwisho wa NASA kuhusu kuruka chombo hicho kurudi kikiwa na watu au bila watu, huenda ukafanyika ndani ya wiki chache.

Lakini hata kama Williams na Wilmore wataweza kurejea mwezi Septemba, hali kama hizo zitatokea katika siku zijazo - haswa kadiri vyombo vya angani vitakavyokuwa vya kisasa zaidi na misheni za kwenda Mwezini na kwingineko.

Mwaka ujao, Victor Glover atasafiri kwenye chombo cha Artemis II, misheni ya kwanza kuondoka kwenye mzunguko wa dunia tangu 1972.

Pia unaweza kusoma

Imetafsiriwa na Rashid Abdallah

Imehaririwa na Maryam Abdalla