Nani atakuwa binaadamu mwingine kutua mwezini?

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES
1969, chombo cha Apollo 11 kiliwapeleka Bus Aldrin na Neil Armstrong kwenye mwezi. Baada ya hapo hadi 1972, Marekani ilipoacha kutuma watu kuchunguza mwezi, watu 10 kutoka Marekani waliweza kukanyaga mwezi kutokana na chombo cha Apollo.
Baada ya zaidi ya nusu karne kupita, hamu ya kwenda mwezini imeibuka upya. Marekani inapanga kutuma wanaanga mwezini, akiwemo mtu mweusi na mwanamke mmoja.
Si Marekani pekee inayojaribu kuweka mguu kwenye mwezi; China na India pia zinapanga safari zao za mwanzo kutuma watu mwezini.
Mpango wa uchunguzi wa anga za juu wa Marekani ulikuwa ni jibu juu ya mafanikio ya Umoja wa Kisovieti, kutuma mwanaanga Yuri Gagarin 1961 kwenda anga za juu.
Kwa sasa si nchi pekee zinazotaka kwenda huko, hata makampuni binafsi yanahusika na yana ajenda zao.
Urusi, China India, Japani na Umoja wa Ulaya wamefanikiwa kutuma satelaiti ndogo au roboti ndogo kutua mwezini, lakini bado hawajapeleka binadamu.
Rasilimali na Kituo

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES
Safari ya kwanza wa kwenda mwezini - ilikuwa tu ni kwenda mwezini, sio kufanya utafiti. Lakini sasa inahusu pia teknolojia ambayo itawawezesha watu kuishi huko, pamoja na jinsi ya kutumia fursa zilizoko.
Mpango wa Marekani wa kwenda mwezini ni safari ya kusafiri zaidi ya mwezini.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
"Wazo lao ni kuanzisha kituo katika mwezi wakati wa kwenda Mars. Na kutumia mwezi kama kituo cha safari," anasema Profesa Namrata Ghoswami kutoka kitivo cha global management chuo kikuu cha jimbo la Arizona, Marekani.
Anaongeza, “kwa sababu ya graviti ndogo katika mwezi, kurusha satelaiti kutoka mwezini itakuwa rahisi kuliko kuzirusha kutoka duniani, ndio maana nchi zinajaribu kutafuta umiliki wa kimkakati wa mwezi.”
Baadhi ya maeneo kwenye mwezi yanapigwa na jua muda wote, kwa hiyo kuna nafasi nzuri ya kuzalisha nishati ya jua. Lengo ni kutuma nishati inayozalishwa mwezini hadi kwenye satelaiti kubwa katika obiti ya chini ya dunia na kupokelewa duniani.
Madini ya salfa na aluminiamu yanapatikana karibu na ncha ya kusini ya mwezi, Mradi wa Utafiti wa Mwezi wa India umethibitisha hilo. Sasa tunaelekea kutafuta vitu zaidi vinavyoweza kusaidia maisha.
Baada ya furaha isiyo na kifani Marekani kuwa wa kwanza kuweka mguu kwenye mwezi, katika miaka ya 1960. Kulikuwa na mazungumzo ya kwenda kwenye nyota. Lakini jambo hilo haliwezi kutekelezwa hivi karibuni.
“Kutoka duniani inachukua siku tatu tu kufika mwezini. Itachukua miezi sita hadi minane kwa watu kwenda sayari ya Mihiri (mars). Kwa hivyo ni hatua kubwa,” anasema Eric Berger, mhariri wa anga za juu katika tovuti ya teknolojia ya Ars Technica.
Kushinda Vikwazo

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES
Kwenda mwezini pia kunahusisha kushinda vikwazo vya kiteknolojia.
Kwanza, tunahitaji roketi yenye nguvu kubeba wafanyakazi wa angani na kuwalinda dhidi ya mionzi.
Mbali na hilo, changamoto nyingine ni kutua salama mwezini. Iwapo kutakuwa na hitilafu ya kiufundi, wanaanga hawatoweza kupata usaidizi kutoka nje na hawatoweza kuendelea na misheni.
Vyombo vya anga vinavyorudi kutoka mwezini - huingia kwenye angahewa ya dunia kwa kasi ya kutisha ya kilomita kadhaa kwa sekunde. Kwahiyo usalama ni jambo la msingi.
Je, itakuwaje ikiwa nchi zitafika kwa pmoja mwezini? Kulingana na Mkataba wa Anga za Juu wa 1967, hakuna nchi inayoweza kudai umiliki wa eneo katika anga ya juu.
"Kwa nchi ambayo itagundua kitu katika mwezi itakuwa na faida ya kwanza. Kwani hadi sasa, hakuna masharti yoyote rasmi ya jinsi ya kugawana rasilimali za mwezini," anasema Bi Goswami.
Mbio mpya za angani

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES
Ifikapo mwaka 2030, China inapanga kujenga kituo cha kudumu kwenye mwezi. Marekani pia ilipanga kujenga kituo cha anga kwenye mwezi 2028, lakini utekelezaji bado uko nyuma ya ratiba.
Mafanikio ya Marekani yanategemea mafanikio ya bilionea Elon Musk, ambaye kampuni yake ya uchunguzi ya Space X bado iko katika uzalishaji wa roketi inayoitwa Starship.
India pia inapanga kuzindua safari itakayokuwa na watu mwaka ujao. India inalenga kujenga kituo cha anga ifikapo 2035 na kutuma wanaanga mwezini ifikapo 2040.
"Programu ya anga ya juu ya China inavutia sana, na tutaona uwezo wao kwa sababu watakuwa wamekamilika," anasema Goswami.
“Natabiri China itakuwa nchi itakayoweza kutua juu ya mwezi katika karne ya 21 kwa sababu ya utafiti wake, maendeleo makubwa na lengo lao," anasema Goswami.














