'Utawala wa Iran unaonekana kuwa thabiti zaidi baada ya mashambulizi ya Marekani na Israel' - Guardian

.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Ayatollah Ali Khamenei ndio kiongozi mkuu wa kidini nchini Iran
Muda wa kusoma: Dakika 7

Kuanzia Tehran hadi Moscow na Gaza, ziara ya leo ya wanahabari inaibua maswali kuhusu ufanisi wa sera za kimataifa zilizopo, mipaka ya mamlaka na matokeo ya ukimya, wakati ambapo dalili za mabadiliko makubwa ya mitazamo ya baadhi ya nchi za Magharibi na wananchi wao kuelekea kwa washriki wao wa jadi zinaonekana.

Tunaanza ziara hii kwa makala iliyochapishwa katika gazeti la Uingereza The Guardian na Simon Tisdall, ambayo inazungumzia mashambulizi ya Marekani na Israel yaliyolenga Iran mwezi Juni 2025, ikiyaelezea kama "majanga ambayo hayakufanikiwa malengo yake yoyote na badala yake yalisababisha madhara hatari, ndani na nje ya Iran."

Tisdall anaanza makala yake kwa kuangazia ongezeko la hukumu za kifo nchini Iran, ambazo hutekelezwa kwa kunyongwa, mara nyingi baada ya kesi za uwongo, kwa kutumia mateso na kukiri kulazimishwa.

Umoja wa Mataifa umenukuliwa ukisema kuwa "zaidi ya watu 600 walinyongwa mwaka huu, na kuifanya Iran kuwa mnyongaji mkuu zaidi duniani ."

Mwandishi anaamini kuwa ongezeko hili linakuja katika muktadha wa kampeni pana ya ukandamizaji kufuatia mashambulizi ya hivi majuzi ya Marekani na Israel, ambayo yaliua zaidi ya watu 900, wengi wao wakiwa raia, na kujeruhi zaidi ya 5,000.

Makala hiyo inabainisha kuwa shambulio hilo lililoongozwa na Israel na Marekani "halikuharibu vifaa vya nyuklia vya Iran kama inavyodaiwa," halikuangusha utawala huo, wala kusimamisha mpango wake wa kurutubisha madini ya uranium. "Kwa hakika, utawala ulionekana kuwa na ujasiri zaidi, kwani Kiongozi Mkuu Ali Khamenei alijibu kwa kampeni iliyoenea ya kukamatwa, shutuma za uhaini dhidi ya wapinzani wake, na matumizi makubwa ya hukumu ya kifo."

Mwandishi anataja kisa cha wanasiasa wa upinzani Behrouz Ehsani na Mehdi Hassani, ambao walinyongwa wiki iliyopita "baada ya kesi zisizozidi dakika tano," hatua iliyolaaniwa na Amnesty International kama jaribio la kukandamiza sauti pinzani wakati wa mzozo wa kisiasa.

Tisdall anaongeza kuwa kwa sasa Bunge la Iran linajadili muswada wa kupanua wigo wa hukumu ya kifo, huku shutuma za kushindwa kwa usalama zikielekezwa sio kwa uongozi, bali kwa "mawakala wa ndani," kufuatia kulengwa kwa mkutano wa siri wa usalama ambapo Rais wa Iran Masoud Pezeshkian alijeruhiwa.

Pia unaweza kusoma
.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Bunge la Iran kwa sasa linajadili mswada wa kupanua wigo wa hukumu ya kifo.
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Makala hiyo inatahadharisha kuwa, shambulio hilo limekuwa na athari za kieneo na kimataifa, ikiwa ni pamoja na kusimamisha ushirikiano wa Iran na wakaguzi wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki, mpasuko mkubwa kati ya Washington na Ulaya, kuimarika kwa watu wenye misimamo mikali ya Iran, na mfano hatari kwa nchi nyinginezo kama vile Urusi kushambulia majirani zao bila ya kuadhibiwa.

Tisdall anasisitiza kwamba mashambulizi hayo yaliegemezwa kwenye hofu na uvumi badala ya taarifa thabiti, "kwani si Israel wala Marekani ambayo imetoa ushahidi kamili kwamba Iran inatafuta kupata silaha za nyuklia."

Tehran, wakati huo huo, inashikilia kuwa haina, wala haina nia ya kumiliki, silaha hiyo, ikisisitiza kwamba urutubishaji wake wa uranium ni kwa madhumuni ya kiraia.

Mwandishi anaibua barua ya onyo iliyoandikwa na mwanafikra wa Kifaransa Montesquieu katika kitabu chake "Barua za Kiajemi" zaidi ya miaka 300 iliyopita, ambamo anafikiria kuibuka kwa silaha za maangamizi ambazo siku moja zingehukumiwa na ulimwengu wote.

Tisdall anaamini kuwa hali hii imetekelezwa kwa kiasi, lakini dhamira ya kimataifa bado ni tete.

Mwandishi anahitimisha kuwa njia ya amani itasalia wazi ikiwa Marekani na Israel zitaamua kupunguza maghala yao ya nyuklia, kuacha kutishia Iran, na kuunga mkono juhudi za kuanzisha makubaliano ya kikanda ya nyuklia, kama ilivyopendekezwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani wa Iran, Mohammad Javad Zarif.

"Je, Donald Trump hatimaye ameanza kuuelewa msimamo wa Putin?

Katika gazeti la The Independent, ambalo limebainisha katika tahariri yake kwamba Rais wa Marekani, Donald Trump ameanza kutambua waziwazi kwamba Rais wa Urusi Vladimir Putin "si mfanyabiashara, bali ni kiongozi anayestawi katika vita na anaamini katika kufufua wazo la kuwa na Urusi Kubwa," hatua ambayo inafanya kukomeshwa kwa vita vya Ukraine "kutegemee mapenzi yake pekee.

Gazeti hilo linasema kuwa Trump alikosea alipofikiri angeweza kumshawishi Putin kusitisha vita kupitia makubaliano ambayo yalijumuisha maneno ya kubembeleza, vitisho vya kutumia nguvu na makubaliano.

Kilichojulikana baadaye, hata hivyo, ni kwamba Kremlin haikuwa na nia ya kufanya mazungumzo, "lakini badala yake ilikuwa na haja ya mara kwa mara ya migogoro ili kuunganisha mamlaka yake ya ndani, hata iwapo italazimika kugharamika kuendelea kumwaga damu."

Gazeti hilo linaunga mkono onyo la hivi majuzi la Trump kwamba anaipa Urusi "siku 10 hadi 12" kuepuka vikwazo zaidi, licha ya muda wake usio na mpangilio. Hata hivyo, inaamini maana ya kisiasa nyuma ya ujumbe huu ni wazi: "Hakuna nafasi ya kuizuia Moscow."

Gazeti hilo linaelezea mzozo wa hadharani kati ya Trump na Dmitry Medvedev, rais wa zamani wa Urusi na mshirika wa Putin, kama dalili ya kuvunjika kwa mawasiliano kati ya Washington na Moscow.

Inaeleza kuwa "mvutano ulifikia kilele" baada ya Trump kuamuru kutumwa kwa nyambizi mbili za nyuklia za Marekani kwenye eneo "karibu na Urusi," kujibu onyo la Medvedev dhidi ya kuhusika moja kwa moja katika mzozo wa nyuklia.

Gazeti hilo linasisitiza kuwa Trump hapo awali alifanya makosa alipotishia kuondoa uungaji mkono wa Marekani kwa Ukraine, lakini kwa bahati nzuri hakufuata. Gazeti hilo linaamini kuwa ingawa kiwango cha uungaji mkono wa sasa bado hakijafahamika, ishara ya msimamo huo mpya inaashiria kubadilika kwa mtazamo wa Trump kuhusu uzito wa hali hiyo.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Trump alifanya makosa siku za nyuma alipotishia kuondoa uungwaji mkono wa Marekani kwa Ukraine, lakini kwa bahati nzuri hakufuata.

Gazeti hilo linasema kwamba kujaribu kuingia makubaliano na Putin huenda kukawa na manufaa mwanzoni, lakini kuliigharimu Washington katika suala la maadili na kanuni, hasa pale Rais wa Ukrain Volodymyr Zelensky alipokabiliwa na kile gazeti lilichoeleza kuwa ni mchezo wa kufedhehesha katika Ikulu ya Marekani Februari 2025.

Anaongeza kuwa Trump anaweza kuwa na jukumu la kuwatahadharisha Wazungu juu ya jukumu lao la kutetea bara lao, lakini hapaswi kufanya hivyo kwa gharama ya haki ya watu huru kupinga uchokozi.

Gazeti hilo linasisitiza kuwa jumuiya ya kimataifa, ikiwemo Marekani, ina wajibu wa kimaadili usioweza kubatilishwa wa kutetea demokrasia, haki za binadamu na haki ya watu kujitawala.

Anasema vita vinaweza kuisha kwa mpigo wa moyo ikiwa Putin alitaka kweli, na kwamba Trump hatimaye anaona wazi kwamba Kremlin ndio sababu kuu ya mzozo huo, kulingana na The Independent.

Mkristo Mzayuni: 'Israeli inahitaji kufungua macho yake'

Katika gazeti la New York Times, David French, mwanasheria wa zamani wa kijeshi ambaye alitumikia Iraq na kujieleza kuwa "Mzayuni Mkristo," aliandika kwamba Israel, licha ya kuwa na haki kamili ya kujilinda baada ya shambulio la Oktoba 7, ilikuwa imeenda mbali sana katika operesheni yake ya kijeshi huko Gaza, "hadi kufikia hatua ya kuwa tishio la kiadili na la kimkakati kwa uwepo wake."

Mwandishi anaamini kwamba jibu la Israel kwa shambulio la Hamas lilikuwa halali, sawa na jibu la Marekani na washirika wake kwa ISIS, lakini anasisitiza kwamba "mateso ya raia wa Palestina yamevuka mipaka ya hitaji la kijeshi, na kwamba njaa inayokuja sio matokeo yasiyoepukika, lakini kosa kubwa la kisiasa na kimaadili."

Mfaransa anatoa tathmini yake juu ya data ya misaada iliyochapishwa na New York Times, ambayo inaonyesha kwamba kiasi cha misaada ya kibinadamu inayoingia Gaza ilizidi tani 200,000 kwa mwezi kabla ya Israel kusimamisha mwezi Machi, na kisha ikapungua hadi viwango vya karibu sifuri.

Hata baada ya marufuku kuondolewa mnamo Mei 2025, mwandishi anabainisha, Mfaransa anaamini kuwa idadi hiyo haijarudi kwa kiwango cha chini kinachokubalika. Anasema jinsi misaada inavyosambazwa leo huongeza mateso kwa raia, hasa wazee, wagonjwa na watoto wanaolazimika kuvuka maeneo hatari ya kijeshi.

Anaongeza kuwa Israel, kwa kuzingatia kusambaratika kwa serikali ya Hamas na udhibiti wa jeshi lake katika Ukanda wa Gaza, imekuwa chombo pekee chenye uwezo wa kuandaa ugawaji wa misaada, lakini imechagua kuutenga Umoja wa Mataifa bila kutafuta njia mbadala yenye ufanisi, "na kuwaacha wakazi kushindwa kabisa kukidhi mahitaji yao ya kimsingi ya chakula."

Mfaransa anaonya kuwa Israel inafanya kile ambacho Hamas inataka: "Mateso ya raia yanaeneza propaganda za vuguvugu hilo, ambalo kwa muda mrefu limejificha nyuma ya hospitali, misikiti na raia ili kutatiza jibu lolote la kijeshi," anasema.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, "Israel iko katika wakati wa nguvu za kijeshi za muda mfupi, lakini udhaifu wa muda mrefu, huku kukiwa na kupungua kwa uungwaji mkono wa umma wa Magharibi.

Mwandishi anasema kuwa Israel inakabiliwa na muda mfupi wa nguvu za kijeshi , lakini udhaifu wa muda mrefu, huku kukiwa na upungufu mkubwa wa msaada wa umma wa Magharibi.

Imetahadharishwa dhidi ya kutafsiri kurudi nyuma huko kama kuunga mkono Hamas, kwani hata Jumuiya ya Waarabu na Umoja wa Ulaya wametoa wito kwa Hamas kusalimu silaha, kuwaachilia mateka, na kuachia udhibiti wa Gaza.

Anasisitiza kuwa Israel haiwezi kumudu kupoteza uungwaji mkono wa nchi za Magharibi, kwani licha ya kumiliki silaha za nyuklia, haifurahii uhuru wa kimkakati unaofurahiwa na nchi kama vile Marekani au Uingereza.

Anaamini kwamba mabadiliko ya sera ya Marekani yanaweza kuwa hatari, hasa ikiwa uungaji mkono kwa Israel utakuwa na masharti ya utambulisho wa chama tawala katika Ikulu ya White House.

"Acheni njaa huko Gaza, acheni kuzungumza juu ya unyakuzi, na mlinde raia," alisema, akibainisha kuwa "kuishinda Hamas hakuhitaji njaa kumuathiri hata mtoto hata mmoja.

Pia unaweza kusoma

Imetafsiriwa na Seif Abdalla