Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Matatizo ya kiuchumi ya China yanamaanisha nini kwa ulimwengu
Kuna msemo kwamba Marekani ikipiga chafya, dunia nzima hupata homa.
Lakini nini kinatokea wakati Uchina haipo sawa?
Nchi hiyo yenye uchumi wa pili kwa ukubwa duniani, na yenye zaidi ya watu bilioni 1.4, inakabiliwa na matatizo mengi - ikiwa ni pamoja na ukuaji wa mwendo wa polepole, ukosefu mkubwa wa ajira kwa vijana na soko la mali yake lipo katika hali mbaya.
Sasa mwenyekiti wa kampuni ya kujenga na kukodesha majumba ambayo inakabiliwa na madeni mengi, Evergrande amewekwa chini ya uangalizi wa polisi na hisa za kampuni hiyo kusimamishwa kwenye soko la hisa.
Ingawa masuala haya yanaonekana kuongeza changamoto kwa Beijing, je yana umuhimu gani kwa ulimwengu wote?
Wachambuzi wanaamini wasiwasi kuhusu uwezekano wa athari za kiuchumi duniani umetiliwa chumvi sana.
Lakini mashirika ya kimataifa, wafanyikazi wake na hata watu wasio na uhusiano wa moja kwa moja na China wanaweza kuhisi angalau baadhi ya athari hizo.
Bila shaka inategemea na wewe ni nani.
Washindi na walioshindwa
Mamia ya makampuni makubwa duniani ka Apple, Volkswagen na Burberry yanaingiza pato kubwa kutoka kwa watumiaji wa soko la China na yataathirika kutokana na watu wa China kupunguza matumizi yao.
Matokeo yake kisha yataathiri maelfu ya wasambazaji na wafanyakazi duniani ambao wanategemea kampuni hizi.
Unapozingatia kwamba China huchangia zaidi ya theluthi tatu ya maendeleo duniani, aina yoyote ya kushuka kwa uchumi wake itatikisa hadi nje ya mipaka yake.
Shirika la ukadiriaji wa mikopo la Marekani Fitch lilisema mwezi uliopita kwamba kushuka kwa uchumi wa China "kunaweka kuwa na athari ya ukuaji kiuchumi " na kupunguza utabiri wake kwa ulimwengu wote mnamo 2024.
Hata hivyo, kulingana na baadhi ya wachambuzi wa masuala ya uchumi, wazo kwamba China ndio kitovu cha ustawi wa dunia limetiwa chumvi.
“Kwa haraka haraka ukipiga hesabu, ndio, China huchangia takriban 40% ya ukuaji wa uchumi duniani,” anasmea George Magnus, mchumi katika Chuo Kikuu cha Oxford.
“Lakini je, ukuaaji huo unamfaidisha nani? China inaendesha ziada kubwa ya biashara yake. Inaingiza bidhaa nyingi nchini mwake kuliko zile inazonunua kutoka kwa nchi zingine, kwa hivyo, ni kwa si kiasi gani China inakua au haikui, zaidi ni kuhusu China kuliko ilivyo kwa dunia yote."
Hata hivyo, watu nchini China hutumia pesa kidogo kwa bidhaa na huduma - au katika ujenzi wa nyumba – inamaanisha kupungua kwa mahitaji ya malighafi na bidhaa.
Mnamo mwezi Agosti, nchi hiyo iliagiza bidhaa kutoka nje karibu 9%, hiyo ikiwa ni kiwango cha chini ikilinganishwa na wakati huo huo mwaka jana - wakati ilikuwa bado chini ya vizuizi vikali vya janga virusi vya corona.
"Wauzaji wakubwa wa bidhaa nje ya nchi kama vile Australia, Brazili na nchi nyingi barani Afrika wataathirika zaidi na hili,” anasema Roland Rajah mkurugenzi wa Kituo cha Indo-Pacific Development katika Taasisi ya Lowy huko Sydney.
Kupungua kwa mahitaji ya bidhaa China pia inamaanisha kwamba bei ya bidhaa mbali mbali zitasalia kuwa chini.
Kwa mtazamo wa mtumiaji katika nchi za Kimagharibi, hilo itakuwa la kufurahisha kwa sababu litasaidaia kupungua kwa bei ambayo haijumuishi kuongezeka zaidi kwa viwango vya riba.
“Hizi ni habari njema kwa watu na biashara ambazo zinakabiliwa na mfumuko wa bei,”Bw Rajah anasema.
Hivyo, katika muda mfupi, watumiaji wa kawaida huenda wakafaidika kutokana na kushuka kwa uchumi wa China.
Lakini kuna maswali ya muda mrefu kwa watu walio katika mataifa yanayoendelea.
Katika miaka 10 iliyopita, China inakadiriwa kuwa imewekeza zaidi ya trilioni moja ya dola za Marekani katika miradi mikubwa ya miundombinu, maarufu kama mpango wa ‘Belt and Road Initiative.’
Zaidi ya nchi 150 zimepokea pesa kutoka kwa China pamoja na teknolojia kujenga barabara, viwanja vyya ndege, mabandari na madaraja.
Kulingana Bw. Rajah, kujitolea kwa China katika miradi hii kunaweza kuanza kuathirika ikiwa matatizo ya kiuchumi yataendelea nyumbani.
“Kwa sasa kampuni za China na benki hazitakuwa na uwezo wa kutoa fedha kote duniani,” anasema.
China na sera zake za kigeni
Wakati kukiwa na uwezekano wa kupungua kwa uwekezaji wa China duniani, bado haijakuwa wazi jinsi gani hali ya uchumi nchini China itakavyoathiri sera zake za kigeni.
China ilio katika hatari zaidi, baadhi ya wachambuzi wanasema, huenda nchi hiyo itataka kurekebisha uhusiano wake na Marekani.
Vikwazo vya biashara vya Marekani vimesababisha kupungua kwa 25% ya bidhaa za China kwenda Marekani katika kipindi cha miezi sita ya kwanza mwaka huu, huku waziri wa biashara wa Marekani Gina Raimondo hivi karibuni akiitaja nchi hiyo [China] kama “isio rafiki” kwa kampuni za Marekani kuwekeza.
Hata hivyo, hakuna ushahidi kueleza China imeanza kulegeza msimamo katika sera zake. Beijing inaendelea kulipiza kisasi kwa vizuizi vyake, mara kwa mara inakashifu "mawazo ya Vita Baridi" ya nchi za magharibi na inaonekana kudumisha uhusiano mzuri na viongozi madikteta wa utawala uliowekewa vikwazo kama vile Vladimir Putin wa Urusi na Bashar Al-Assad wa Syria.
Wakati huo huo, maafisa wengi kutoka Marekani na Umoja wa Ulaya wanaendelea kusafiri hadi China kila mwezi ili kuendeleza mazungumzo kuhusu biashara baina ya pande hizo mbili
Ukweli ni kwamba watu wachache tu wanaweza kutofautisha baina ya matamshi ya China na sera yake.