Nchi ambayo vitunguu ni ghali zaidi kuliko nyama

A woman opens a bag of onions in Quezon City, Manila on January 10, 2023

Chanzo cha picha, ROLEX DELA PENA/EPA-EFE/REX/Shutterstock

Maelezo ya picha, Kilo moja ya vitunguu ilifikia dola 11 nchini Ufilipino

Katika maeneo mengi duniani vitunguu ni chakula kikuu huku nyama ikiwa ya anasa zaidi, lakini nchini Ufilipino bei ya vitunguu imepanda sana kuliko ile ya kuku na nyama ya ng'ombe.

Tabia ya kukaanga na vitunguu saumu na vitunguu maji katika nchi ya Asia ilianza wakati wa ukoloni wa Uhispania, ambao ulidumu kati ya 1521 na 1898 na kuathiri sana mapishi ya vyakula vya nchi ya Asia.

Kwa karibu mwezi mmoja, hata hivyo, vitunguu vimekuwa bidhaa ya anasa kwa Wafilipino. Baada ya kupanda kwa bei, bidhaa hiyo inagharimu zaidi ya nyama aina nyingi tu.

Kilo moja ya vitunguu vyekundu na vyeupe ilifikia takriban $11 wiki hii, huku kuku mzima angeweza kununuliwa kwa karibu $4.

Hiyo ni ghali kuliko kima cha chini cha kila siku cha mshahara nchini Ufilipino, ambacho ni zaidi ya $9.

Kutokana na kupanda kwa bei, mamlaka za nchi hiyo zimekamata hata shehena zisizo halali za vitunguu. Mapema Januari, vitunguu vya thamani ya $310,000 kutoka Uchina vilinaswa baada ya jaribio la kuvisafirisha kwa magendo vilivyoandikwa kama nguo.

Kutokana na kupanda kwa bei, mamlaka za nchi hiyo zimekamata hata shehena zisizo halali za vitunguu.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Mapema Januari, vitunguu vya thamani ya $310,000 kutoka Uchina vilinaswa baada ya jaribio la kuvisafirisha kwa magendo vilivyokuwa na vibandiko vya nguo.

Katika mitandao ya kijamii, Wafilipino wamechapisha jumbe nyepesi za kuikosoa serikali, ambayo wengi wanaona kuwa inafaa kulaumiwa kwa hali ya sasa.

"Kwaheri Chokoleti, karibuni vitunguu swaumu. Sibuya yaani [vitunguu] vina uwezo wa kuwa zawadi nzuri ya kuleta nyumbani nchini Ufilipino," Mfilipino mmoja anayeishi Marekani alichapisha ujumbe huo kwenye Twitter.

"Tunaleta vitunguu badala ya chokoleti kutoka kwa safari yetu ya Saudi Arabia," aliandika mwingine.

Pia katika safari ya Marekani, mtumiaji mwingine alishirikisha picha ya jagi lenye vitunguu vya unga: "Kwa vile kitunguu ni kama dhahabu Ufilipino, nilitaka kununua hivi ili kuleta nyumbani na kutoa kama zawadi. Lakini nimetembelea maduka makubwa matano na akiba yote ya bidhaa hii imeisha. Nilimuuliza msichana mmoja wa mauzo kilichotokea na akasema kwamba 'watalii wa Ufilipino walikuwa wamenunua vyote'".

Nicholas Mapa, mwanauchumi mkuu katika benki ya ING anayeishi katika mji mkuu wa Ufilipino, Manila, alisema kuwa baadhi ya mikahawa imeacha kuuza bidhaa ambazo zinahitaji vitunguu – menyu ambazo kawaida huwa na vitunguu kama vile burger, kwa mfano, hakuna tena.

"Hawawezi kupanga bei ya bidhaa zao ipasavyo au hawawezi kutoa kipata vitunguu," aliambia BBC kupitia barua pepe.

Biashara zingine zinatafuta njia mbadala. Mpishi Jam Melchor, mwanzilishi wa Vuguvugu la Kuhifadhi Urithi wa Kitamaduni wa Ufilipino, amekuwa akitafuta mbadala.

Ameamua kutumia aina ya kitunguu cha asili kiitwacho ‘lasona’, ambacho ladha yake ni tofauti na ile ya kitunguu cha kawaida na pia ni kidogo - saizi ya zabibu.

"Vitunguu ni muhimu sana kwa vyakula vya kienyeji. Huingia katika karibu kila mlo tunaotayarisha hapa. Ni kiungo muhimu katika kila vyakula vya Kifilipino," Melchor aliongeza.

Kwa nini vitunguu vimekuwa ghali sana huko Ufilipino?

Nicholas Mapa anatoa angalau sababu mbili zenye kuchangia kupanda kwa bei.

Makadirio kutoka kwa Idara ya Kilimo yaliyotolewa mwezi Agosti yalionyesha kuwa nchi ingezalisha vitunguu vichache ambavyo vitahitajika. Mavuno, hata hivyo, yalikuwa mabaya zaidi kuliko ilivyotarajiwa, kwani Ufilipino ilikumbwa na kimbunga kikubwa kati ya Agosti na Septemba.

"Kwa bahati mbaya, uagizaji wa vitunguu ulianza kuchelewa, baada tu ya bei kupanda - na karibu sana na kipindi cha mavuno, ambacho ni Februari", alielezea mwanauchumi.

Katika wiki ya kwanza ya Januari, serikali iliidhinisha uagizaji wa karibu tani milioni 22 za vitunguu ili kujaribu kurejesha bei ya bidhaa hiyo chini na kudhibiti bei.

Street food in Cebu

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Chakula cha mitaani huko Cebu: ushawishi wa Kihispania umesababisha kuweka vitunguu katika milo mingi ya nchini Ufilipino

Kwa baadhi ya wataalam kama Fermin Adriano, ambaye hapo awali alikuwa mshauri wa Idara ya Kilimo, ilikuwa kushindwa sana kwa utawala wa sasa.

Kwa maoni yake, kwa vile serikali ilijua kuwa uzalishaji wa ndani ni mdogo, ilipaswa kuagiza bidhaa kutoka nje ya nchi za kutosha ili angalau zilingane na mahitaji yaliyotarajiwa.

A person puts onions on a scale in Quezon City, Metro Manila, Philippines on January 10, 2023

Chanzo cha picha, ROLEX DELA PENA/EPA-EFE/REX/Shutterstock

Maelezo ya picha, Pamoja na vitunguu saumu, vitunguu maji ni viungo muhimu kwa vyakula vya Ufilipino.

Bidhaa ya tatu inayozalishwa zaidi duniani

People carrying bags of onions in Quezon City, Metro Manila, Philippines on January 10, 2023

Chanzo cha picha, ROLEX DELA PENA/EPA-EFE/REX/Shutterstock

Maelezo ya picha, Kimbunga kilichoikumba Ufilipino katikati ya mwaka wa 2022 pia kiliathiri uzalishaji

Cindy van Rijswick, mchambuzi wa matunda na mboga mboga huko Rabobank, anasema kwamba, kiutamaduni, Ufilipino ni nchi inayoagiza vitunguu kutoka nje - hutumiwa zaidi kuliko inavyozalishwa.

Hitaji hili linabadilikabadilika sana: kutoka kilo milioni tano pekee mwaka 2011, anaeleza, hadi kilo milioni 132 mwaka 2016.

"Nchi kwa kawaida hununua bidhaa hii kutoka India, China na Uholanzi, kulingana na bei na upatikanaji", mchambuzi alisema.

Mojawapo ya sababu za utegemezi huu ni kwamba uzalishaji mwingi wa vitunguu nchini Ufilipino, kutokana na hali ya hewa, ni wa aina ambazo hazidumu kwa muda mfupi.

Hii ni tofauti na kile kinachotokea, Van Rijswick anaongeza, katika baadhi ya mikoa ya Kaskazini mwa Ulaya na Amerika ya Kaskazini, ambapo, kwa hali nzuri, vitunguu vinaweza kuhifadhiwa hadi mwaka.

"Katika sehemu nyingi za dunia, vitunguu ni miongoni mwa mboga tatu zinazotumiwa zaidi. Ndio maana vitunguu pia ni mboga ya tatu inayozalishwa kwa wingi duniani. Ni nyanya na matango pekee ndizo zinazozalishwa zaidi."

Kupanda kwa bei ya vitunguu pia ni shida mahali pengine

Kwa kiasi kidogo, bei ya vitunguu imepanda katika nchi nyingine kadhaa. Mfano mmoja ni Brazili, ambayo ilikuwa na ongezeko la juu zaidi katika 2022: 130.14%, kulingana na takwimu rasmi.

Miongoni mwa sababu za ongezeko hilo ni kupunguzwa kwa ardhi ya kilimo na gharama kubwa za uzalishaji, kwani vifaa kama vile mbolea na viuatilifu viliathiriwa na viwango vya ubadilishaji wa fedha kimataifa na vita nchini Ukrainia.