Lishe: Zifahamu faida 5 kuu za vitunguu

Getty

Chanzo cha picha, Getty Images

Kitunguu ni nini? Katika mimea, vitunguu ni sehemu ya familia ya Liliaceae , pamoja vitunguu saumu, na vitunguu maji.

 Ingawa thamani yake iko chini ya vitunguu saumu, vitunguu vina viungo vyenye ufanisi mkubwa katika kuboredha afya ya mwili.

Vitunguu huwa sehemu ya vyakula mbali mbali tunavyokula kila siku, vikiwemo vile vinavyoliwa vikiwa vibichi kama vile kachumbari, na saladi, vilivyookwa au kuchemshwa.

 Kipande cha gramu 80 cha kitunguu (kibichi) huwa na:

  • Gramu 0.8 za protini
  • Gramu 6.4 za wanga
  • Sukari gramu 5.0
  • Gramu 1.8 za nyuzinyuzi(fiber)
  • Miligramu 2.0 za vitamin C.

Kitunguu chenye ukubwa wa kati , chenye gramu 80, ni sawa na kiwango cha milo mitano ya vyakula vyenye kutia nguvu unavyofaa kula kwa siku

Getty

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ulaji wa mara kwa mara wa vitunguu hupunguza hatari ya kuvunjika kwa nyonga

1. Onion ina mchanganyiko wa kemikali zinazozuiakuharibika kwa seli nzuri za mwili

Vitunguu vimejaa kemikali za mmea, ikiwa ni pamoja na flavonoids, ambazo zote zina uwezo wa kuzuia kuharibika kwa seli na kuzuia majeraha mwilini (anti-inflammatory).

 Vinapoliwa mara kwa mara na katika kiwango kinachofaa, mchanganyiko huu wa kemikali za mme unaweza kukulinda dhidi ya magonjwa ya kudumu kama ile saratani na kisukari.

Ukweli ni kwamba vitunguu huwa vina aina tofauti 25 za virutubisho vya flavonoids na ni miongoni mwa vyakula vyetu vyenye virutubisho vingi.

 Vitunguu pia vina madini ya salfa. Vimeonyesha kuwa kinga ya aina fulani za saratani

2. Vitunguu vinaweza kuchangia afya bora

Mojawapo ya viungo vya flavonoids katika vitunguu, quercetin, kina sifa ya kulinda seli za mwili na kuzuia majeraha mwilini.

 Tafiti zinasema kwamba ulaji wa vitunguu unaweza kupunguza hatari ya kupatwa na ugonjwa wa moyo kwa kushusha shinikizo la damu, kudhibiti viwango vya mafuta na kupunguza majeraha mwilini.

g
Maelezo ya picha, Vitunguu vimejaa kemikali za mimea, ikiwa ni pamoja na flavonoids, ambazo zinazuia uharibifu wa seli na kuzuia majeraha mwini

3. Vitunguu vinaweza kusaidia afya ya utumbo

Kujumuishwa kwa vitunguu katika mlo kuhahusishwa na iuzito wa mifupa. Hii huenda inatokana na kiungo kinacholinda seli za mwili dhidi ya sumu zinazoua seli, jambo ambalo hupunguza uharibifu wa seli na hivyo kupunguza kukonda kwa mifupa.

 Utafiti uliochunguza athari za vitunguu miongoni mwa wanawake wanaokaribia na waliofikia ukomo wa hedhi unaonyesha kuwa wanawake wanaokula mara kwa mara vitunguu walipunguza hatari ya kuvunjika mifupa ya nyonga.

 Utafiti mwingine wa wanawake wenye umri wa kati unaonyesha kuwa unywaji wa juice ya vitunguu unapunguza kukonda kwa mifupa na badala yake huongeza uzito wa mifupa.

g
Maelezo ya picha, Kujumuishwa kwa vitunguu katika mlo kunahusishwa na kuongezeka kwa uzito wa mifupa

Vitunguu vina kiwango cha hali ya juu cha nyuzinyuzi au fiber, hususan nyuzinyiz ambazo haziwezi kusagwa na tumbo la chakula, ambazo zinahitajika katika kuimarisha afya ya utumbo. 

Ingawa hatuwezi kusaga vyakula vyenye nyuzinyuzi za bakteria , bacteria wanaoishi katika utumbo wetu wanaweza kufanya hivyo na kuzitumia kama petroli ya kuongeza idadi yao na kuzalisha kile kinachoitwa fatty acids (SCFAs).

Tafiti zinaonyesha kuwa SCFA hizi ni muhimu katika kuimarisha afya ya utumbo na hivyo kusaidia mfumo wetu wa usagaji wa chakula na ule wa kinga kufanya kazi vyema.

5. Vitunguu, hupambana na bakteria

Tafiti zinaonyesha kuwa vilipotumiwa katika dawa za kikohozi, na mafua , viunguu vilikuwa na viungo vya kupambana na bakteria ...Zaidi ya hayo, ni vitunguu vilivyohifadhiwa kwa muda mrefu vilivyoonekana kuwa na ufanisi zaidi.

Je vitunguu ni salama kwa kila mtu?

Mzio wa vitunguu ni nadra, lakini baadhi ya watu wanaweza kuupata. Matokeo yake, watu wenye mzio wanaweza kupata matatizo ya usagaji wa chakula, ikiwa ni pamoja na kiunguliwa na gesi tumboni.

 Vitunguu vina FODMAP, aina ya wanga na nyuzinyuzi ambazo mifumo ya usagaji chakula wa baadhi ya watu hauwezi kuzimudu.

Jinsi ya kuchagua na kutunza vitunguu

Vitunguu vinapaswa kuwa visafi na vyenye Ngozi ngumu na laini. Epuka vitunguu vinavyoonyesha dalili ya kuoza.

Vitunguu vinapaswa kuhifadhiwa katika chumba chenye joto la kawaida, mbali na mwangaza na katika eneo lenye hewa ya kutosha . Vitunguu vya rangi ya manjano, na nyeundu, vinaweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu kuliko vitunguu maji.

 Vitunguu vyoto vinapaswa kuhifadhiwa tofauti na viazi, kwani vinaweza kufyonza unyevunyevu wa viazi na gesi ya ethylene, inayosababisha viazi kuoza haraka. Usitunze vitunguu katika kifaa au bakuli la chuma, kwani inaweza kuondoa rangi yake.

 Kuhifadhi kwenye friji vitunguu vilivyokatwa kunaweza kuondoa sehemu kubwa ya ladha yake.

Kiungo cha sulfate, ambacho hutengenezwa wakati seli za kitunguu huzinapokatwa na kupaa ndizo zinazosababisha mtu kutoa machozi.

 Kupunguzwa kwa uzalishaji wa kiungo hiki, unaweza kupoza kitunguu kwa karibu dakika thelathini kabla ya kukikata.