Waislamu waliobadilisha jinsia na kukaribishwa msikitini hawana uhakika wa siku za baadaye

.
Maelezo ya picha, Taasisi ya Kiislamu ya Al-Fatah huko Yogyakarta, Indonesia ina karibu wanachama 63, ambao wote wamebadili jinsia

Mustakabali wa taasisi pekee ya jumuiya ya Kiislamu nchini Indonesia kwa wanawake waliobadili jinsia uko hatarini baada ya kiongozi wake, Shinta Ratri, kufariki dunia mwezi Februari - na serikali inasema haiwezi kuunga mkono hilo.

Kuna wanawake 63 waliobadilisha jinsia zao ambao huhudhuria mara kwa mara taasisi ya jamii cha Al-Fatah, ambayo inawaruhusu kuomba, kujifunza Qurani, kujifunza ujuzi au kujumuika kwa urahisi bila kuhukumiwa kwa jinsi walivyo.

Rini Kaleng ni mmoja wao.

Baada ya kuamka kila asubuhi, yeye hujipodoa na kuvaa wigi lake jeusi analolipenda zaidi kabla ya kuchukua mkoba na kuelekea kwenye mitaa ya jiji la kihistoria la Yogyakarta wenye shughuli nyingi.

Anatembea kwa maili na maili, akicheza muziki kutoka kwa spika yake ya Bluetooth na kuimba ili kupata riziki. Lakini siku za Jumapili, safari yake inaisha kwa ziara ya alasiri kwenye taasisi ya Al-Fatah kusoma Quran.

"Ni mahali salama ambapo tunaweza kusali," asema Bi Rini, ambaye amekuwa akienda huko tangu 2014.

Akiwa mtoto, Bi Rini ambaye alizaliwa mwanaume alijisikia raha zaidi kucheza na wasichana badala ya wavulana. Angevaa kama msichana, akicheza na vinyago vya jikoni na kujifanya bibi na marafiki zake.

Baada ya kujitokeza kama aliyejibalisha jinsia na kuwa mwanamke, wazazi wake na kaka zake tisa walikubali utambulisho wake. Sasa, anatambuliwa na watu mitaani wanaomwona akiimba na kucheza.

"Unaweza kusema mimi ni mtu Mashuhuri hapa," anacheka.

.
Maelezo ya picha, Rini Kaleng
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Bibi Rini alijua kwa mara ya kwanza kuhusu taasisi hiyo ya Kiislamu ya wanawake waliobadilisha jinsia zao kutoka kwa rafiki yake ambaye pia alitaka kusomea dini.

Aligundua jamii nzima ya wanawake kama yeye ambao walikuwa na ndoto sawa.

Katika misikiti, mara nyingi alikuwa anaangaliwa vibaya anapoenda kuswali. "Sio lazima walitukubali. Kwa hivyo nilienda mahali pa Shinta Ratri, nilipoelekezwa na rafiki yangu," anasema.

"Taasisi nyingi za Kiislamu hazikubali watu waliobadili jinsia," anasema Nur Ayu, mlezi wa kituo hicho.

"Hapa, tuko huru... huru kuja kama mwanamume au mwanamke, yoyote yule tunachojisikia vizuri." Shinta Ratri alikuwa mmoja wa waanzilishi wa kituo hicho cha jumuiya ya Al-Fatah.

Mwanaharakati mashuhuri na kiongozi wa kituo hicho tangu 2014, Bi Shinta alishirikiana na mashirika mengi yasiyo ya faida ili kuendeleza haki za watu waliobadilisha jinsia nchini Indonesia.

Lakini mwezi Machi, alifariki akiwa na umri wa miaka 60 kutokana na mshtuko wa moyo, siku tatu baada ya kulazwa hospitalini.

Idadi ya wengi walioumizwa sana na kifo chake ni pamoja na waliobadilisha zao.

.

Chanzo cha picha, ULET IFANSASTI/GETTY IMAGES

Bi Nur anaelezea Bi Shinta kama mwanga elekezi, na mtu wa karibu zaidi aliyenaye kwa familia. Bila yeye, uahisi tu taasisi hiyo ina "ombwe na ukiwa".

Kifo cha Bi Shinta kimeweka mustakabali wa taasisi hiyo ya jamii mashakani. Jengo hilo linamilikiwa na familia ya marehemu kiongozi - na wameiomba taasisi ya Al Fatah kuhama.

"Lazima tuweze kuendelea bila Shinta na kujitegemea," anasema Bi Nur.

YS Albuchory, katibu wa Taasisi hiyo ya Kiislamu, anaelezea wamepokea msaada kutoka kwa marafiki katika jamii na mashirika ya haki za binadamu, ndani na kimataifa.

Lakini kukubalika kwa jumuiya ya waliobadilisha jinsia katika taasisi za kidini za Indonesia ni kwa kiwango cha chini sana.

Ukweli ni kwamba jamii "bado inakataa hadhi ya kijamii na kidini ya watu waliobadili jinsia", mmoja wa wahusika wa taasisi hiyo anasema.

.
Maelezo ya picha, Wanachama wa Al-Fatah Islamic Center wakishiriki dua ya pamoja kabla ya kufuturu wakati wa Ramadhani

Rully Mallay, mmoja wa viongozi wa taasisi hiyo, anasema Al Fatah inashukuru kwa "aina yoyote ya uhalali ambayo tumepewa".

Ana matumaini kwamba siku moja, jumuiya ya watu waliobadili jinsia itakubalika zaidi katika nchi yenye kujumuisha kila mmoja kama Indonesia.

Tumaini hilo linamtia motisha yeye na marafiki zake kuendeleza kituo hicho.

“Uislamu unapaswa kuwa na uwezo wa kutoa nafasi kwa mtu yeyote kuweza kuabudu kwa uhuru kulingana na njia za dini,” Bi Rully anasisitiza.

.
Maelezo ya picha, Bi Rosidah (kulia) akiwafundisha wanafunzi wawili waliobadili jinsia kusoma Quran

Changamoto sasa ni kutafuta eneo jipya - na pesa za kufadhili. Na inahitaji kuwa katika eneo ambalo litawakubali.

Majirani wa sasa huko Yogyakarta wamekuwa wakikaribisha.

Mmoja wao ni Bi Rosidah, mwanajamii wa eneo hilo ambaye yeye hajabadilisha jinsia yake na amekuwa akifundisha huko kwa zaidi ya mwaka mmoja.

"Nilikuwa na shughuli nyingi, lakini kwa sababu nilikuwa na hamu ya kutaka kujua, nilienda kutembelea," anasema Bi Rosidah.