Sheria Itakayowasimamia watu wenye jinsia mbili yawasilishwa kwa mwanasheria mkuu Kenya

Maelezo ya video, Sheria Itakayowasimamia watu wenye jinsia mbili yawasilishwa kwa mwanasheria mkuu Kenya

Jopo linaloangazia mabadiliko ya kisheria na usimamizi kuhusu watu wanaobadili jinsia nchini Kenya sasa linawasilisha ripoti yao ya mwisho kwa mwanasheria mkuu , Kariuki Kihara .

Kulingana na ripoti ya awali jopo hilo lilikuwa limependekeza kwamba sheria inafaa kutoa alama maalum ya watu waliobadili jinsia katika stakhabadhi zote za kisheria nchini Kenya.

Je ilikuwaje serikali ya Kenya ikapiga hatua hiyo?

Hiki hapa kisa cha mtoto ambacho kilishinikiza mazungumzo kuhusu haki ya watu wenye jinsia mbili nchini Kenya.

Video: Judith Wambare