Trinitite: Vito vya ajabu vilivyotokana na mlipuko wa kwanza wa nyuklia duniani

ghghgh

Chanzo cha picha, CESAR MENOR-SALVAN

Maelezo ya picha, Vito vya Trinitite vina muonekano kama madini

Trinitite sio madini wala sio kitu cha asili. Ni kitu ambacho kiliundwa kutokana na tukio la kusikitisha katika kihistoria la mlipuko wa kwanza wa nyuklia - Julai 16, 1945, huko Alamogordo, (New Mexico), Marekani.

Wakati mwisho wa Vita vya pili vya dunia unakaribia. Mradi wa Manhattan uliokuwa ukiendelea tangu 1941, kipindi cha Rais Franklin D. Roosevelt, alipohofia uwezekano wa Ujerumani kuunda aina mpya ya silaha za maangamizi, aliidhinisha mradi wenye changamoto kubwa ya kiufundi na kisayansi katika historia.

Mradi huo ulihusisha wanafizikia, wanakemia, wahandisi, wanahisabati, na maelfu ya wafanyikazi katika juhudi za kukimbizana na wakati.

Mafanikio ya kiufundi ya mradi wa Manhattan yalitoa msukumo kwa maendeleo ya viwanda na teknolojia ya Marekani. Pia, yalipanda mbegu za Vita Baridi, kutokana na matunda yake makubwa.

Bomu la Gadget

esdfrtgyhjukl;./

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Gadget lilikuwa bomu la kwanza la nyuklia katika historia

Bomu la Gadget ulikuwa ni mfano wa kwanza wa bomu la nyuklia kufanya kazi. Mnamo Julai 15, 1945, Gadget lilikuwa lipo tayari kulipuliwa katika jaribio la utata. Bomu lenye plutonium-239, lilikuwa na nguvu ambazo hazijapata kushuhudiwa kabla.

Plutonium -239 inayolipuka kwa urahisi inatengenezwa kwa miale ya urani na neutroni. Plutonium haipatikani katika maumbile ya dunia. Inapatikana katika mabaki ya urani katika vinu vya nyuklia.

Moja ya changamoto za mradi huo ilikuwa ni kupata plutonium safi ya kutosha kutoka kwa urani. Hivyo walitumia Reactor B ya kiwanda cha siri cha Hanford (Washington) cha uzalishaji wa plutonium.

Ulikuwa mtambo wa kwanza wa nyuklia wa kibiashara kwa ajili ya uzalishaji wa plutonium, ukimilikiwa na kampuni ya DuPont, ambayo ilikataa faida zake na kujitenga na eneo hilo ili isihusishwe na maendeleo ya bomu. Kwa sasa eneo hiyo ni makumbusho.

Saa 11:29 alfajiri, Julai 16, 1945, bomu la Gadget lililipuliwa katika jangwa la Jornada del Muerto. Huo ulikuwa mlipuko wa kwanza wa nyuklia katika historia – likiachia kele za uzito wa kilotoni 19. Lilikuwa na nguvu kuliko ilivyotabiriwa, liliharibu baadhi ya vyombo vya kisayansi vilivyo umbali uliodhaniwa kuwa salama.

Baada ya mlipuko huo, Kenneth Bainbridge, mkurugenzi wa kisayansi wa mradi huo, alipayuka, "sasa sisi ni washenzi wa kweli."

Robert Oppenheimer, alisema haya yalikuwa maneno sahihi zaidi ambayo yalisemwa baada ya mlipuko.

Mabomu mawili yaliyofuata - Little Boy na Fat Man (matoleo ya Gadget), yaliua watu wapatao 214,000 katika miji ya Japan ya Hiroshima na Nagasaki. Takribani nusu walikufa kutokana na milipuko na wengine kutokana na mionzi.

Joto liliyeyusha mchanga wa jangwani

errtetrt

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Bomu hilo lilikuwa sawa la lile la Fat Man lililodondoshwa Nagasaki, Japan

Halijoto ya mlipuko wa bomu la Gadget lilizidi lile ya uso wa jua. Joto liliyeyusha mchanga wa jangwani. Vioo vilinyesha katika maeneo ya umbali wa mamia ya mita.

Baada ya ulipuaji kwisha, watafiti waliona ardhi imefunikwa na vioo vyenye rangi ya kijani. Na vioo vingine kama vito. Walikusanya sampuli ambazo zilihifadhiwa kama kumbukumbu ya tukio la kihistoria. Baadhi ya vioo vilitumiwa kutengeneza vito vya kipekee.

Baadaye waligundua kuwa hilo lilikuwa wazo baya, kwani vito vya trinitite vilikuwa na mionzi mikali kiasi cha kusababisha ngozi kuchomeka.

Leo, vito hivyo vimepoteza mionzi yake na vinaweza kutumika vikiwa salama. Lakini bado ni ushahidi wa mlipuko wa nyuklia.