Mapacha wazaliwa kutoka kwenye viinitete vilivyogandishwa zaidi ya miaka 30 iliyopita

Getty

Chanzo cha picha, NATIONAL EMBRYO DONATION CENTER

Maelezo ya picha, Lydia Ann na Timothy Ronald Ridgeway walizaliwa tarehe 31 Oktoba,2022

Watoto wachanga mapacha wamezaliwa katika jimbo la Tennessee kutoka kwenye viinitete vilivyogandishwa kwenye barafu kwa miaka zaidi ya 30 iliyopita.

Inaaminiwa kuwa kuwa ni rekodi mpya ya viinitete vilivyogandishwa kwa muda mrefu zaidi kuwahi kuleta matokeo ya kufanikisha kuzaliwa kwa watoto hai .

Viligandikwa katika barafu ya takriban -128C (-200F) katika kimiminika cha nitrogen tarehe 22 Aprili 1992.

Rachel Ridgeway, mama wa watoto wanne kutoka eneo la Oregon, alijifungua mapacha hao tarehe 31 oktoba. Baba yao, Philip Ridgeway, alisema kuwa "inashangaza -akili’’

Lydia Ann na Timothy Ronald Ridgeway huenda wakaweka rekodi mpya , kulingana na kituo cha kitaifa cha utoaji wa viinitete (NEDC), ambalo ni shirika la kibinafsi ya kidini linalosema limesaidia kuzaliwa kwa watoto 1200 kutokana na msaada wa viibitete.

Mtu wa awali aliyeshikilia rekodi ya shirika la NEDC, Molly Gibson, alizaliwa mwaka 2020 kutokana na kiinitete ambacho kilikuwa kimegandishwa kwa zaidi ya miaka 27

"Uamuzi ... wa kuasili viinitete hivi unapaswa kuwahakikishia wagonjwa ambao wanawasis wasi iwapo kutakuwa na mtu yeyeto ambaye anataka kuasili viinitete vilivyobuniwa miaka 5, 10, 20 iliyopita," Dkt John David Gordon, aliyehamisha kiinitete.

"Jibu hilo ni ndio!"

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

 Viinitette vya mapacha hao vilibuniwa kutoka kwa wanandoa wasiojulikana kwa kutumia njia ya uzazi wa IVF. Mwanaume alikuw ana umri wa miaka 50 na ushee na inaripotiwa kuwa vilitegemea mtoaji wa yai la uzazi mwenye umri wa miaka 34.

Viinitete vyao vilitunzwa katika maabara ya uzazi iliyopo katika mwambao wa magharibi mwa Marekani hadi mwaka 2007 wakati wana ndoa walipovitoa kama msaada kwa kampuni ya NEDC iliyopo Knoxville, Tennessee kwa ajili ya wanandoa wengine kuvitumia badala yao.

Mtaalamu wa viinitete katika kliniki inayoshirikiana na NEDC ya Southeastern Fertility baadaye alihamishia viibnitetehivyo katika mfuko wa uzazi mwaka .

Katika taarifa yake, NEDC ilisema inatumai taarifa hii "itawatia moyo wengine kuweza kupata uzoefu wa kuasili viinitete kwa ajili yao wenyewe".

Ni watoto wa kwanza wa familia ya Ridgeway – ambao wamepatikana kwa njia ya IVF au kwa njia msaada.

Familia hiyo ina watoto wengine wanne wenye umri wa kati ya mwaka mmoja na minane.

"Nilikuwa na umri wa miaka mitano wakati Mungu alipowapatia uhai Lydia na Timothy, na amekuwa akitunza maisha hayo tangu wakati huo ," Philip Ridgeway aliiambia CNN kutoka kwenye nyumba ya familia.

 "Ukweli ni kwamba, ndio watoto wetu wakubwa zaidi, ingawa ni watoto wetu wadogo zaidi ."

"Kuna kitu cha kushangaza akilini kuhusu hili ," aliongeza.