Je kuna hatari gani ya kupata mtoto baada ya kutimu umri wa miaka 40 na zaidi?

mtoto

Chanzo cha picha, Getty Images

Shangazi yangu alijifungua mtoto akiwa na umri wa miaka 45, rafiki yangu alijifungua akiwa na umri wa miaka 47, jirani yangu akiwa na umri wa miaka 43, hii ndio misemo inayozunguka miongoni mwa wanawake na katika kanda nchi za kiarabu

Licha ya hili, kauli hizi haziwezi hazitengani na onyo kwa wanawake dhidi ya kuchelewa kupata ujauzito, " hawataweza kuwa na uwezo wa kuwa na watoto baada ya umri fulani, lakini wanaume wanawza kupata watoto katika umri wowote ."

Je ni upi usahihi wa wa onyo hili? Je umri wa miaka arobaini ndio wa mwisho kwa wanawake katika maisha ya wanawake pekee?

Dokta Hind Abdel Salam aliiambia BBC kwamba wanawake wengi wanatarajia kwamba iwapo watafikia umri huu hawataweza kuwa na uwezo wa kuwa na watoto, na wakati mwingine hutishwa na wale wanaowazingira kwamba fursa za ujauzito hazipo, na hili sio kweli kabisa , kwani ukweli ni kwamba inategemea mwanamke mwenyewe, kuna wanawake wanaoweza kupata ujauzito katika umri wa miaka arobaini na minane na baadaye .

Umri wa uzazi

Unaweza pia kusoma:

Kuna tofauti katika uwezo wa kuzaa wa wanawake na wanaume, jambo muhimu ambalo linahusiana na uwezo wa kuzaa. Kwa wanawake, kuna kupungua taratibu kwa uwezo wake wa kuzaa kuanzia umri wa miaka 35. 

Sababu ya hili ni kwamba mwanamke huzaliwa na mayai yake yote ambayo anaweza kuyatengeneza katika kipindi chake chote cha maisha na idadi hii hupungua kadri miaka ya umri wake inavyokwenda . 

Mwanamke huzaliwa na zaidi ya mayai ya uzazi milioni na hupungua hadi 400,000 katika umri wa kubarehe na kufikia hadi 25,000 wakati anapofikia umri wa miaka 37, kwani wanawake wengi hupoteza 90% ya mayai ya uzazi katika umri huu, hadi mwanamke anapotimiza umei wa miaka 51 huwa na mayai 1000.

Hivyo basi fursa ya kupata ujauzito hupungua taratibu kila mwezi, na kufikia %5 miongoni mwa wanawake wenye umri wa miaka 40 na zaidi, ikimaanisha kuwa fursa ya mimba bado ipo, lakini kwa kiwango cha chini. Hii pia inatofautiana kwa mwanamke na mwanamke.

kwa upande mwingine, viwango vya uwezo wa kuzalisha kwa wanaume hupungua saw ana inavyotokea kwa wanawake , kinyume na inavyofahamika kwa wengi, lakini hupun gua baadaye na kwa utaratibu zaidi kuliko wanawake. Uwezo wa kuzalisha wa mwanaume hupungua kati ya umri wa miaka 40 na 45.

Tofauti na mayai katika wanawake, mbegu za uzazi za mwanaume hutengenezwa katika kipindi chote cha maisha yake, lakini ubora wa mbegu hizi hupungua kadri mwanaume anapoendelea kuku ana kuwa mtu mzima na uzazi wa mtoto huhusiana na ubora way ai na mbegu ya uzazi kwa pamoja.

G

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, ,“Hakuna tiba au uwkiziuizi cha kisayansi kwa mwanamke kupata uujauzito baada ya umri wa miaka 40. Suala linahusiana na haja ya ya kupata usaidizi zaidi wa kimatibabu na kiafya

Mimba katika umri wa zaidi ya miaka 40

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Doaa Al-Saft aliiambia BBC BBC, "Baada ya kufikia umri wa miaka 40 yapata miezi sita, nilibaini kuwa ’’ Nilikuwa mjamzito na sikutarajia kabisa ." nilipatwa nilipigwa na mshangao’’

Doaa alimficha kila mtu taarifa ya ujauzito wake kwasababu aliogopa kauli za maoni ya watu kwamba " wakati mwingine zinaweza kutofurahisha, ambapo wakati mwingine huwa wanasema bado una nguvu ya kuwa na watoto, au unapaswa kufikiria kuhusu kuwaoza watoto wako badala ya wewe kufikiria kupata watoto. Kutokana na hayo Duaa alikuwa akivaa mavazi makubwa katika kipindi chote cha ujauzito.

 Familia yake ilimuunga mkono na kumsaidia na kumpatia ushauri na kumwambia kuhusu wanawake wengine waliojifungua wakiwa na umri wa miaka 40 na wana afya njema na watoto wao wana afya njema , lakini baadhi ya marafiki madaktari walichangia katika kumtisha Duaa .

Duaa aliniambia kuhusu safari ndefu na ya kuchosha akili aliyopitia katika kumtafuta daktari ambaye angemsaidia, na anasema:

 ‘’Daktari niliyemuona wa kwanza aliniambia kwamba wewe una umri mkubwa na kwamba unapaswa kuzalishwa kabla ya kuingia katika mwei wat isa wa ujauzito kutokana na hofu ya matatizo unayoweza kuyapata.

Mwingine aliniandikia madawa mengi ya kuimarisha ujauzito wangu, akidai kuwa mimba yangu una uwezekano wa kuharibika kawababu mimi nina umri mkubwa,na ninapaswa pia kupewa dawa ya kuifanya damu iyeyuke "Niliogopa sana. Ninafahamu kwamba baada baada ya miaka arobaini, ubora wa mayai ya uzazi hupungua kwa kiwango kikubwa, jambo linaloweza kuathiri afya ya kijusi , kama vile kuzaliwa kwa mtoto mwenye hali Down syndrome, kuzaliwa na kasoro za viungo, au kuwa matatizo mengine’’

 Hofu kuhusu kijusin haikuwa pekee iliyotawala uzoefu wa Dua’a, lakini piaalijihofia binafsi, hususan kutokana na msisitizo wa daktari ambaye ’’alimtisha kwamba anakabiliwa na uwezekano wa kupata kisukari na shinikizo la damu’’

Umri bora

Doaa alijifungua mtoto wake wa tano, Ammar, mapema mwaka huu, n ani mwenye afya nzuri. Doaa ana afya njema. Anasema, "Hakuna umri fulani wa kujifungua, lakini kuna matayarisho mazuri kwa ajili ya kujifungua. Nilijifungua mara nne kabla ya Ammar, lakini mara hii ni tofauti kabisa.

 ‘’Ninahisi kukomaa zaidi na mwenye uzoefu kuliko awali . Mara hii licha ya hofu zote, Ninafurahia uzoefu sana’’."

Wakati mwingine Doaa huhisi kwamba Ammar anabahati na uzoefu wake na uzoefu wa awali, lakini wakati mwingine anamhurumia , "Ninapokwenda kwake mpangilio wa muda wake unakuwa ni kwenda kwenye chanjo, ninahisi kuwa nimekuwa mtu mzima zaidi ya wanawake wengine wanaonizingira .

 Ninaogopa kumuacha mapema, lakini wakati huo ninihisi kuwa niko katika nafasi bora ya kumtunza kuliko wengine’’.

 Tuliwauliza wanawake na wanaume katika nchi kadhaa za kiarabu kuhusu umri unaofaa kupata mtoto , na wote walizungumzia kuhusu miaka 20 na ushee kwa mwanamke . Na wote wakaafiki kuwa mwanamke hawezi kupata mroro akiwa na zaidi ya umri wa miaka thelethini na mitano, jambo ambalo zio kweli.

 Daktari Hind Abdel Salam anasema, hakula chochote cha kuhofia katika umri huu , unayohitaji ni huduma bora za matibabu , “Iwapo kuna tabia kama vile uvutaji wa sigara au unywaji wa vilevi, mama anapaswa kuzisitisha , pamoja na kuimarisha kiwango cha sukari na uzito ili view vya kawaida.

 Dokta Hind anawashauri wanawake wenye umri wa miaka 40 kuendelea na mazoezi ya mwili , kupata virutubisho sahihi vya mwili na wanahitaji kuendelea kutumia vitamini muhimu wakati wa ujauzito , na kumeza folic acid ili kuepuka matatizo yoyote ya kiafya au kuwa na vijusi vyenye kasoro.

 Madaktari wanasisistiza kuwa wanaweke wenye umri wa zaidi ya miaka 40 wana uwezekano mkubwa wa mimba zao kuharibika baada ya kupata uzazi kwa njia ya IVF wakilingangishwa na wanawake wenzao waliopata watoto wakiwa na umri wa miaka thelathini na ushee au miaka ishirini na ushee waliopata watoto kwa njia ya upandikizaji au hata kwa njia ya kawaida.

 Hayo pia hutokea inapokuja katika uwezo wa kunyonyesha, ambao wanawake wanaendelea kuwa nao, sawa na uwezo wa kuzaa inategemea mwanamke mmoja na mwingine, uwezo wa kutunga mimba unategemea mwanamke na mwanamke.