Vita vya Ukraine: Zifahamu rasilimali 5 zilizopokwa na Urusi huko Ukraine mpaka sasa

Na Svitlana Dorosh, BBC Ukraine

Ukraine

Chanzo cha picha, Getty Images

Wakati wa vita vya kuiteka Crimea, kuanzia mwaka wa 2014, Urusi ilinyakua mamia ya rasilimani na amana za Ukraine. Kwa hesabu za kawaida, thamani ya rasilimali hizo inaweza kuwa kati ya Dola trilioni 12.5 hadi trilioni 15.

Ukraine inapoteza mafuta, gesi, makaa ya mawe, chumvi, chuma, dhahabu, uranium, granite, manganese na lithiamu kutokana na uvamizi wa Urusi.

Je, matokeo ya hasara hizi ni yapi na nchi itaweza kuanza tena uzalishaji baada ya ukombozi wa maeneo yake yenye rasilimali hizo?

Jeshi la anga la Ukraine lilipokea raatifa za kipekee kutoka kwa Taasisi ya Sayansi ya Jiolojia ya Chuo cha Kitaifa cha Sayansi cha Ukraine juu ya kiasi cha hasara kilichopatikana mpaka sasa.

Vita vya malighafi

Mapema mwanzoni mwa 2023, wakati Warusi waliteka eneo la Soledar, ambayo ina mwamba ulio karibu na Bakhmut wenye utajiri wa chumvi, kulikuwa na uvumi kwamba mkuu wa PMC "Wagner" Yevgeny Prigozhin alihitaji eneo hilo ili kujipatia madini.

Shirika la Reuters liliandika kuhusu uwezekano huo wa kutekwa eneo hilo ili kupora chumvi ya Ukraine.

Vyombo vya habari vya serikali ya Urusi pia vinaandika juu ya akiba kubwa ya rasilimali za madini katika mikoa iliyotekwa na Urusi, ikijadili matarajio ya maeneo haya na wataalam.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Wanasayansi wanasema kwamba nchini Ukraine kuna aina zipatazo 120 za madini ambazo zina umuhimu wa kiviwanda. Kwa kuongeza, kuna amana za madini adimu 21 yaliyo kwenye orodha ya madini 30 yaliyofafanuliwa na Umoja wa Ulaya kama "malighafi muhimu". Ni muhimu kwa maendeleo ya nishati ya "kijani". Hizi ni lithiamu, cobalt, scandium, grafiti, tantalum, niobium na nyingine.

"Takriban asilimia tano ya hifadhi ya dunia ya "malighafi muhimu" iko nchini Ukraine, ambayo inachukua asilimia 0.4 tu ya uso wa Dunia," Naibu Waziri wa Ulinzi wa Mazingira na Maliasili Svitlana Grinchuk alisema katika mkutano wa Tume ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa.

Kwa kuinyima Ukraine kupata rasilimali zake za asili, Shirikisho la Urusi lilisababisha uharibifu mkubwa wa mabilioni ya dola.

Taasisi ya Sayansi ya Jiolojia ilikadiria kuwa Ukraine kwa sasa haidhibiti zaidi ya amana 700 kati ya zaidi ya 2,160 zilizopo. Hiyo ni, karibu theluthi moja. Ziko katika maeneo yaliyochukuliwa na Urusi au karibu na mstari wa mbele wa vita. Kati ya nyingi hizi ni rasilimali tano muhimu zilizo kwneye mikono ama himaya za warusi.

1. Makaa ya mawe

"Hasara kubwa zaidi ambayo Ukraine imepata ni akiba ya madini yanayoweza kuwaka: hidrokaboni na makaa ya mawe," Msomi Shehunova aliiambia BBC Ukraine.

Karibu robo ya amana za mafuta na gesi za Ukraine ziko katika maeneo yanayokaliwa na jeshi la Urusi, lakini hali ya makaa ya mawe ni mbaya zaidi: Ukraine imepokwa zaidi ya 80% ya amana zake za makaa ya mawe.

Aidha, kulingana na Waziri wa Nishati wa Ukraine Herman Galushchenko, robo ya migodi ya makaa ya mawe inayomilikiwa na serikali ni miongoni mwa migodi iliyotekwa.

2. Madini ya chuma

Inaaminika kuwa Ukraine ina amana kubwa zaidi duniani ya madini ya chuma, anasema mkurugenzi wa Taasisi ya Sayansi ya Jiolojia.

Mnamo mwaka wa 2014, amana za bonde la chuma la Kerch, lilitekwa huko Crimea.

Mnamo 2022, Urusi pia ilikamata amana za wilaya za madini ya chuma za Bilozersky na Pryazovsky katika mikoa ya Zaporizhzhia na Donetsk. Akiba ya madini ya wilaya ya Priazovsky pekee inakadiriwa kuwa tani bilioni tatu.

Mnamo mwaka wa 2014, Ukraine ilipoteza karibu 100% ya malighafi ya kaboni kwa utengenezaji wa carbonate ya sodiamu, 90% ya sawdust, zaidi ya 80% ya amana za malighafi, zaidi ya 95% ya amana za refractory clay, pamoja na msingi wa malighafi ya uzalishaji wa bromini , oksidi ya magnesiamu, soda, hafnium, na mengine.

Ukraine

Chanzo cha picha, INSTITUTE OF GEOLOGICAL SCIENCES OF THE NATIONAL ACADEMY OF SCIENCES OF UKRAINE

Maelezo ya picha, Ramani kuonyesha madini katika maeneo ya Mashariki na Kusini mwa Ukraine yalivyokuwa wakati wa mwanzo mwa uvamizi wa Urusi.

3. Dhahabu

Hifadhi nyingi za dhahabu Ukraine ziko katika maeneo yaliyotekwa. Zinatofautiana katika viwango vya kuendelezwa na asili, haswa, hifadhi ya Bobrykivskoye katika mkoa wa Luhansk, hifadhi ya Surozske karibu na Berdyansk katika mkoa wa Zaporizhzhya, pamoja na hifadhi kadhaa katika mkoa wa Donetsk.

4. Chumvi na Manganese

Chumvi ni muhimu. Kila mtu hutumia na ukweli kwamba ni Ukraine mwamba wa chumvi Ukraine umekuwa ukizalisha chumi kwa mamia ya miaka.

Taifa hilo lina machimbo 15, theluthi moja ambayo ina leseni. Lakini kwa miaka kumi iliyopita, mahitaji yote ya chumvi yalihudumiwa na hifadhi moja ya Artemivskoye huko Soledar. Hata kabla ya uvamizi, uchimbaji wa chumvi huko Solera ulikuwa umesimamishwa, na hii ilisababisha uhaba mkubwa wa chumvi.

Hivi sasa, hifadhi moja tu ya Drohobytsky katika mkoa wa Lviv huzalisha chumvi kwa ajili ya soko la ndani, anasema Stella Shehunova. Hifadhi ya kipekee ya Solotvy huko Transcarpathia ilikumbwa na mafuriko mnamo 2010 na ikaharibika vibaya.

Kwa muda mrefu Ukraine ilikuwa inachukuliwa kama nchi yenye hifadhi kubwa ya manganese, ambayo ni muhimu kwa ajili ya maendeleo ya madini. Hifadhi ya Veliko-Tokmak ya madini ya manganese katika mkoa wa Zaporizhzhia sasa iko katika maeneo yaliyochukuliwa.

Nikopol na Marganets katika mkoa wa Dnipropetrovsk, ambapo manganese huchimbwa, ni maeneo yanayokumbwa na makombora ya mara kwa mara.

Ukraine

Chanzo cha picha, INSTITUTE OF GEOLOGICAL SCIENCES OF THE NATIONAL ACADEMY OF SCIENCES OF UKRAINE

Maelezo ya picha, Hifadhi kwenye mwamba wa chumvi katika mkoa wa Donetsk zinaonyeshwa kwa rangi ya machungwa

5. Madini yenye thamani kubwa ya lithium

Kwa mujibu wa serikali, akiba ya lithiamu nchini Ukraine ni takriban tani 500,000. Uzalishaji wake haujaanzishwa, lakini mipango ilikuwa kufanya hivyo.

Urusi iliteka angalau hifadhi za madini haya: Shevchenkivske katika mkoa wa Donetsk na hifadhi ya madini tata ya Kruta Balka katika mkoa wa Berdyansk. Hifadhi za madini ya Lithium katika Mkoa wa Kirovohrad zimesalia chini ya udhibiti wa Ukraine.

Kwa Urusi, lithiamu ni kipande cha keki, kwani haijachimbwa kwenye eneo lake. Hata mwaka mmoja uliopita, afisa wa Wizara ya Viwanda na Biashara ya Shirikisho la Urusi, Vladyslav Demidov, alithibitisha shida ya lithiamu kwa Urusi ni "kubwa", kwani Argentina na Chile ziliacha kuuza nje, na Bolivia ilibaki kuwa muuzaji pekee.

Urusi pia inaagiza kaolin, na kabla ya vita nchi ya Ukraine ndio ilikuwa muuzaji mkuu. Hivi sasa, hifadhi katika mkoa wa Donetsk zimetekwa, na "viongozi" wa watu wanaojiita "DNR", kama ilivyoripotiwa na rasilimali za mtandao na wanazungumza juu ya mipango ya kuanza tena uchimbaji madini.

Rasilimali gani za kimkakati ambazo hazijatekwa?

Kabla ya vita, Ukraine ilikuwa moja ya nchi kumi kubwa zinazozalisha zaidi uranium duniani.

Kuna hifadhi za uranium katika maeneo yasiyodhibitiwa ya mikoa ya Mykolaiv, Kharkiv, Donetsk na Luhansk ambayo bado haijaendelezwa na Ukraine.

Lakini hifadhi kubwa zaidi iko katika eneo linalodhibitiwa, katika mkoa wa Kirovohrad. Ikiwa Urusi ingeweza kuchukua hifadhi kubwa zaidi ya uranium barani Ulaya, ingeimarisha nguvu zake katika soko la mafuta ya nyuklia, Stella Shehunova anasisitiza.

Kwa miaka mingi, Ukraine iliuza madini yake kwa bei nafuu kwenda Urusi. Tangu uhuru, kulikuwa na mipango ya kuanzisha viwanda vya usindikaji na uzalishaji wa mafuta, hii ingepunguza utegemezi kwa wazalishaji wa Kirusi wa TVEL.

Nini athari za kupokwa huku kwa rasilimali na Je, nini kinafuata?

Waziri wa Nishati wa Ukraine Galushchenko alisema kuwa uzalishaji wa makaa ya mawe ulipungua kwa asilimia40%. Mnamo Septemba 2022, serikali ilipiga marufuku kabisa usafirishaji wake nje ya nchi.

Majira ya baridi yaliyopita, Ukraine ilishikilia hifadhi ya makaa ya mawe ya ndani, lakini itaweza kufanya hivyo majira ya yajayo ya baridi? Uhaba wa makaa ya mawe uliibuka mnamo 2014, wakati vikosi vinavyounga mkono uvamizi wa Urusi vilipochukua sehemu ya mikoa ya Donetsk na Luhansk.

Ukraine pia iliacha kuuza nje gesi.

Kulingana na kampuni ya ushauri ya GMK Center, mauzo ya chuma pia yalipungua kwa asilimia 42%.

Gennadiy Ryabtsev, mkurugenzi wa miradi maalum katika kituo cha kisayansi na kiufundi cha "Psyche", anaamini kwamba vita vya sasa vinaongeza mashaka matarajio ya matarajio yao na umuhimu wa uchimbaji wa madini. Hata baada ya ukombozi wa maeneo yaliyotekwa.

Kwanza, haiwezekani kurejesha kikamilifu kwa mfano, migodi ya makaa ya mawe, ambayo mengi yalitelekezwa hata kabla ya vita. Pili, mtaalam huyu anasema, kutakuwa na matatizo na uzalishaji wake sababu sehemu kubwa ya makampuni ya biashara huko Donbass yameharibiwa, na karibu nusu ya vituo vya mafuta vya Kiukreni, ambavyo vilifanya kazi hasa kwenye sekta ya makaa ya mawe vimesimama.

Tatu, kama Ryabtsev anavyosema, inaweza isiwe faida kuanza tena uchimbaji na uendelezaji wa madini kwa ajili ya kuuza nje kutokana na ushindani mkubwa duniani.

Itakuwa na maana ya kuchimba madini yale tu ambayo yanahitajika sana duniani au ambayo ni muhimu kimkakati kwa Ukraine kwa miongo kadhaa ijayo.

"Vita vimeleta pigo kubwa sana kwa uchumi wote wa kitaifa. Kwa sababu ya uwezekano mkubwa wa kutoirejesha kikamilifu, kutakuwa na haja ya kuendeleza maeneo mengine ya sekta za uzalishaji, haswa, chakula na usindikaji, tehama na sekta ya huduma," Ryabtsev wa BBC alihitimisha.