Hypersonic: Makombora yanayotumiwa na Urusi na jinsi yanavyoweza kubadilisha vita vya siku zijazo

Chanzo cha picha, Getty Images
Vita nchini Ukraine huenda zaidi ya kile kinachoenedelea ndani ya mipaka yake.
Pia wakati mwingine huwa uwanja wa nguvu za silaha, katika tukio hili Urusi au NATO, kujaribu silaha kwa lengo la kubadilisha vita vya siku zijazo kama tunavyojua.
Matumizi ya Urusi ya makombora ya hypersonic ni thibitisho tosha
Alizitumia kwa mara ya kwanza mwanzoni mwa uvamizi, ikiashiria mara ya kwanza ya matumizi ya silaha hizi katika vita vyovyote.
Na baada ya miezi kadhaa bila ripoti kwamba yalitumika, walitambua matumizi mapya Alhamisi hii, Machi 9, kama sehemu ya mashambulizi makali dhidi ya Ukraine ambayo yamesababisha vifo vya watu tisa na uharibifu mkubwa wa miundombinu.
Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Urusi Igor Konashenkov, alikiri kwamba walishambulia maeneo muhimu ya miundombinu ya kijeshi ya Ukraine kwa kutumia silaha za masafa marefu zinazolenga kwa usahihi wa hali ya juu, pamoja na makombora ya hypersonic ya Kinzhal.
Hata hivyo rais wa Urusi Vladmir Putin amewahi kusisitiza siku za nyuma kuwa nchi yake inawekeza kwenye makombora ya hypersonic, ingawa mataifa mbalimbali yenye silaha kama Marekani, Iran na China pia yanashiriki kuharakisha upatikanaji wa silaha hizo zenye uwezo wa kulenga kwa mwendo wa kasi.
Makombora ya hypersonic ni makombora ya aina gani?
Kinzhal, ni jina lililopewa kombora la hypersonic linalotumiwa na Urusi, likimaanisha "dagger" kwa Kihispania, yaani kombora lililo na muundo wa ncha kali na hatari.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Serikali ya Urusi inasema ndege hizo zinaweza kuruka kwa kasi ya zaidi ya kilomita 6,000 kwa saa na kulenga shabaha ya hadi umbali wa kilomita 2,000.
Roketi hizi zina urefu wa mita 8 na pia zinasifika kwa uwezo wake wa kubadilisha mwelekeo hata likiwa tayari lishafyatuliwa kwa mashambulizi.
Sifa kuu ya aina hii ya silaha ni kwamba inakwenda kwa kasi kubwa karibia kilomita 1.6 kwa sekunde.
Zinaweza pia kubeba vilipuzi vya kawaida au vichwa vya nyuklia na kurushwa kutoka angani, baharini au nchi kavu.
Mwandishi wa maswala ya usalama wa BBC Frank Gardner, amesema Kuna aina mbili za silaha hizi: Makombora ya masafa marefu na masafa mafupi.
Frank amesema kombora la cruiser, linalotumiwa na Urusi na ambalo pia Urusi inayamiliki kadhaa yanaweza kurushwa kutoka kwa ndege na kulenga shabaha iliyo umbali wa zaidi ya kilomita 1,900, huku ile ya glide inayorushwa kutoka angani na kurudi ardhini kwa njia isiyotabirika.
Hata hivyo, wataalam wamehoji iwapo kweli makombora hayo yataleta mabadiliko, angalau katika muda mfupi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Je, yana tofauti gani na makombora mengine?
Kwa kweli, teknolojia ya hypersonic sio mpya.
Makombora ya ICBM yaliopo katika maghala ya nyuklia duniani yanaweza kufikia kasi hii.
Tofauti kubwa ni kwamba wakati makombora haya yanaweza kuruka kutoka bara moja hadi jingine , urukaji wake unaweza kutabirika, lakini makombora ya kizazi kipya yanaweza kubadili mwendo wake kulingana na hali yakidumisha kasi yake

Chanzo cha picha, REX SHUTTERSTOCK
Tishio kwa usalama wa kimataifa
Wataalamu wanaonya kwamba silaha mpya zinazoundwa za makombora ya hali ya juu ambayo Urusi inatayarisha, kwa mfano yale ya China na Marekani, ni tishio kubwa kwa usalama wa dunia.
Urusi imeripoti kuwa makombora yake ya hypersonic yanaweza kuweka vichwa vya nyuklia, jambo ambalo, iwapo ni "kweli au la," huongeza wasiwasi na kupunguza mawasiliano ya , kulingana na mhandisi wa masuala ya angani Iain Boyd wa Chuo Kikuu cha Colorado Boulder nchini Marekani.
"Kasi kubwa ya silaha hizi huongeza hatari ya hali kwa sababu inapunguza sana wakati wa azimio lolote la kidiplomasia la dakika ya mwisho," Boyd aliandika katika makala katika gazeti la The Conversation.
"Ushawishi wa kudhoofisha unaosababishwa na makombora ya kisasa ya hypersonic labda ni hatari kubwa zaidi," Boyd anasema.
Mtaalam huyo pia alitoa maoni kwamba Marekani na washirika wake "wanapaswa kuorodhesha silaha zao za hypersonic ili kufanya mataifa kama Urusi na Uchina kujadili na kukuza mbinu ya kidiplomasia katika kushughulikia silaha hizi.












