Nilivyotafuta asili yangu katika makaburi ya Algeria

Chanzo cha picha, MAHER MEZAHI
Katika mfululizo wetu wa barua kutoka kwa waandishi wa habari wa Kiafrika, Maher Mezahi anaandika kuhusu kile ambacho kutafuta mizizi ya familia yake kumemfunza.
Nje kidogo ya Skikda, jiji linalopendeza la Mediterania kando ya bahari ya mashariki ya Algeria, familia yangu kubwa inamiliki shamba ambalo liko kwenye mteremko.
Kwa mama yangu na ndugu zake, ardhi ilikuwa njia nzuri ya kutoroka kutoka kwenye nyumba yao iliyo katikati mwa jiji.
Katika likizo ndefu za majira ya kiangazi mashambani, kwa uangalifu walichuna peasi zenye maji mengi, wakiwasha moto na kuvumbua michezo ya ubunifu wakicheza na binamu zao
Kwa kizazi changu, kutembelea ardhi kwa kawaida kulimaanisha siku bila ishara ya simu ya mkononi na kuepuka buibui wa bustani wenye mistari ya machungwa ambao walikuwa na ukubwa wa kiganja changu.
Hata hivyo, sote tunakubaliana kwa kauli moja katika kutambua thamani ya ardhi, hasa kwa sababu ya kilele cha mteremko.
Njia yenye uchafu iliyopinda inaongoza hadi juu, ambapo makaburi ya familia yetu yamekaa kwa amani.
Sauti tu za majani yenye harufu nzuri kutoka kwa mti wa mkaratusi wa karibu huvunja utulivu.
Kila safari ya familia kwenda Skikda, daima huwekwa alama na sisi kutembelea wale ambao wametangulia.
Kundi zima la watu ambao walikuwa na maana kubwa kwangu sasa wanapumzika juu ya mlima, bibi na babu yangu mzaa mama.
Baada ya kukaa nao kwa muda, huwa natafuta mahali pa kupumzika kwa babu yangu, Ahmed.
Maandishi ya rangi ya kijani kibichi kwenye jiwe dogo ambalo hutumika kama kaburi lake yanaonesha kwamba alizaliwa mnamo 1845.
Hunigusa kila wakati kuwa hii ndiyo sehemu ya mbali zaidi ninayoweza kuchimba tena katika historia yangu ya binafsi.

Chanzo cha picha, MAHER MEZAHI
Si jambo la kawaida hata kidogo kwa watu katika nchi yangu au katika bara langu kuweza kupata makaburi ya mababu zao vizazi vinne kwenda juu, na ninakubali upesi na kuthamini upendeleo huu kwangu.
Kwa kukosekana kwa rejista za kisasa za manispaa na vyeti vya kifo, wengi wetu hutegemea ushuhuda wa mdomo ili kujenga miti ya familia zetu.
Katika wiki chache zilizopita, nimekuwa nikipitia anuani zangu za simu na nikachukua kura ya maoni kutoka kwa wenzangu ili kuona uzoefu wao husika ulikuwa ukifuatilia asili yao.
Wenzake nchini Ghana na Afrika Kusini walithibitisha kuwa zoezi hilo lilikuwa la mdomo zaidi na lilitoka kwa wajomba au ndugu wa babu na babu - wangeweza kupanda mti wa familia lakini kufikia vizazi vitatu tu juu yao.
Wanawake walioachwa
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Rafiki mmoja huko Ethiopia aliniambia kwamba katika sehemu za nchi yake "watoto wanalazimika kukariri vizazi vilivyo juu yao".
Tamaduni ya kutaja pia inawakumbuka baba na babu.
Pia najua kutoka kwa marafiki kwamba ni desturi nchini Misri kwa watoto kupewa majina ya kwanza ya baba na babu kama majina ya kati.
Hatahivyo, mbinu kama hizo zinaweza kuwa duni na mara nyingi ni za uzalendo, ikimaanisha kuwa wanawake wa zamani wana uwezekano mkubwa wa kusahaulika kuliko wenzi wao.
Nyakati nyingine, mimi hutamani habari nyingi zilizorekodiwa zinazopatikana kwa watu mahali pengine ulimwenguni.
Nchini Ufaransa, kwa mfano, serikali imeweka kidijitali na kupakia hati muhimu kama vile vyeti vya ndoa, kuzaliwa na kifo kwenye hifadhidata inayopatikana kwenye tovuti ya serikali.
Huko Uingereza na Wales kuna rekodi za kuzaliwa, ndoa na vifo vyote vilivyosajiliwa hadi 1837.
Kwa bahati mbaya, ninaamini kwamba bado tuko miongo kadhaa kutoka kwa raia wa Kiafrika kupata ufikiaji kamili wa hati za kiraia za dijiti kwa kiwango kikubwa.
Lakini kwa nini ni muhimu?
Kuna msemo kwamba "kama hujui unatoka wapi, hujui uendako".
Nimeuliza sana swali hilo katika miezi michache iliyopita.
Moja ya faida kuu za kujifunza historia yako ya kibinafsi ni kwamba unaweza kujielimisha kuhusu wewe mwenyewe.
Ukiwa na maelezo sahihi, unaweza kupata asili ya vipengele vyako mwenyewe, historia ya matibabu au sifa za binafsi.
Pia niko katika hatua hiyo ya maisha yangu ambapo ninaanza kufikiria juu ya vizazi vijavyo na umuhimu wa kupitisha utambulisho wa kitamaduni.
Lakini nadhani somo muhimu zaidi nililojifunza kwa kutazama historia yangu binafsi lilikuwa uhusiano wa kina wa mahali nilipo.
Sio lazima kuhusu bendera, nchi au itikadi. Badala yake, ninakumbuka sehemu hiyo ya ardhi huko Skikda, na jinsi imeilea familia yangu moja kwa moja na kunilea kwa njia isiyo ya moja kwa moja, kwa zaidi ya karne moja sasa.
Nakumbuka ule mti wa mikaratusi, na jinsi pengine ulivyotoa kivuli kwa babu wa babu yangu, Ahmed.
Uelewa huo ni wa kunyenyekea kwa sababu unaniweka moja kwa moja katika mzunguko wa maisha, na pia huleta kiwango cha shukrani ambacho kinaweza kubadilisha kabisa namna ninavyoishi.















