Nyayo zenye utata zinazopinga kile tunachofahamu kuhusu chimbuko la mwanadamu

Chanzo cha picha, Per Ahlberg
Nyayo zilizogunduliwa katika kisiwa cha Ugiriki cha Crete zinaibua maswali na utata mkubwa kuhusu asili ya wanadamu.
Zikiwa zinajulikana kama nyayo za Trachilos, ziligunduliwa mwaka 2002 na mwanakiolojia kutoka Poland Gerard Gierlinski, lakini utafiti mpya unaonyesha kuwa ndio ushahidi wa zamani zaidi wa wanadamu wa zamani wa aina hiyo .
Utafiti uliochapishwa Oktoba 11 katika nakala ya sayansi na kikundi cha kimataifa, unapinga nadharia kuwa hominins (neno linatumiwa na wanadamu wa sasa na mababu zetu wote) walitokea barani Afrika kabla ya sehemu zingine.
Kutokea Afrika
Watafiti kwa kiasi kikubwa wanaamini nadharia kuwa Afrika ndio mwanzo wa mwanadamu.
Kulingana na nadharia hii, wanadamu walianzia katika bara hilo kabla ya kuhama kwenda sehemu zingine za dunia kulikoanza chini ya miaka milioni mbili iliyopita.
Lakini kikundi cha watafiti wanaongozwa na mtafiti kutoka Sweden Per Ahlberg wanapinga nyakati hizo wakidai kuwa nyayo hizo au alama hizo za miguu ni za miaka milioni sita iliyopita.

Chanzo cha picha, Getty Images
Hii inazifanya nyayo hizo kuwa za miaka milionia 2.5 zaidi ya zile zilizodhaniwa kuwa za zamani zaidi ya Laetoli zilizogunduliwa nchini Tanzania mwaka 1976.
Ugunduzi huo uliofanywa barani Afrika umekuwa muhimu katika kubaini chanzo cha wanadamu.
Pamoja na alama hizo za nyayo ya miguu kumekuwa na ugunduzi kadhaa barani Afrika katika kipindi cha miaka 100 iliyopita, ikiwemo fuvu la Sahelanthropus, anayekadiriwa kuishi brani Afrika miaka milioni saba iliyopita.
Ulaya imekuwa na ugunduzi mdogo wa mifupa kama hiyo.
Kipi kiliacha nyayo huko Crete?
Per Ahlberg alikuwa miongoni mwa kikundi ambacho mwaka 2017 kilichapisha nakala ya kwanza kuhusu nyayo za Trachilos - chapisho la oktoba 2021 liliongeza miaka kutoka milioni 5.7 hadi miaka milioni 6.05.
Kwenye nakala ya kwanza Ahlberg na wenzake waliamua kuwa nyayo hizo zilifanana na zile za hominin hasa kuhusu jinsi kidole kikubwa kilionekana kukaribiana na vingine kinyumie na miguu ya sokwe.

Chanzo cha picha, Getty Images
Lakini ugunduzi huo uliopokelewa na shaka na watafiti wengine na kuibua maswali kuhusu ni mbinu gani zilitumiwa kuchunguza nyayo hizo na wengine kupinga wakisema hizo hata hazikuwa nyayo halali.
Wanasayansi wanaamini kuwa sokwe wa kale waliibuka katika kipindi kinachojulikana kama Miocene karibu miaka milioni 23 na million 5 iliyopita.
Wanasayansi wamepata ushahidi wa sokwe wasio wanadamu waliozurura ulaya, kwa hivyo kuna uwezekano kuwa waliacha nyayo huko Crete kwa mujibu wa Robin Crompton, mtaalamu wa anthropolojia chuo cha Liverpool nchini Uingereza.

Chanzo cha picha, Per Ahlberg
Ahlberg anasema hakuna shaka kuwa familia yetu ya Homo sapien ilibukia Afrika karibu miaka 300,000 iliyopita. Dhana ya Homo sapien kutokea Afrika imeandikwa kwa njia bora. Swali hapa ni iwapo wanadamu wote walitokea Afrika. "Labda haikuwa hivyo kulingana na utafiti wetu kuwa wanadamu wa kale huenda walianzia Kusini mwa Ulaya na Afrika Mashariki," Ahlberg anaongeza.
Badala ya kupinga kabisa suala la wanadama kuibukia Afrika, Ahlberg anasema kuna uwezekano kuwa mababu zetu huenda walisambaa kwenda ulaya mapema kuliko vile tunaamini kwa sasa. Mwaka 2017, mwaka ambao pia nakala ya kwanza kuhusu nyayo za Trachilos ilichapishwa, mtafiti mjerumani Madelaine Bohme kutoka chuo cha Tubingen aligonga vichwa vya habari.
Alitangaza ugunduzi kuwa mwanadamu na sokwe wa mwisho haukufanyika Afrika bali Ulaya. Bohme na kundi lake la watafiti walidai kuwa kiumbe walichokiita Graecopithecus, kiliishi eneo la Balkan miaka milioni 7.18 na 7.25 iliyopita, kikiwa cha kwanza kuliko mwanadamu wa kale wa kwanza aliyetembe akiwa amesimama.
"Uchunguzi wetu haupingi historia ya kuibuka kwa wanadamu baada ya miaka milioni 5, lakini kile kilifanyika kabla ya wakati huo," anasema Bohne.
Nyayo za Trachilos zina umuhimu gani?
Ahlberg anasema hakuna shaka kuwa familia yetu ya Homo sapien ilibukia Afrika karibu miaka 300,000 iliyopita. Dhana ya Homo sapien kutokea Afrika imeandikwa kwa njia bora,

Chanzo cha picha, Universidad de Tubingen
Wizi wa nyayo
Nyayo za Trachilos hata zimewavutia wasiokuwa wanasayansi.
Nyayo nane kati ya hizo ziling'olewa kutoka kwa jiwe na kuibwa wiki chache baada ya ungunduzi wao kutangazwa mwaka 2017.
Mwalimu mmoja wa shule ya upili baadaye alikamatwa na polisi nchini Ugiriki na nyayo hizo zikapatikana.













