Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi kubwa tano za soka Ulaya jioni hii (20.08.2022)
Chelsea wanamtaka kweli Harry Maguire. Tetesi zimeendelea leo baada ya jana Chelsea kuwasiliana na Man Utd kuona kama kuna uwezekano kwa nahodha huyo kuhamia Chelsea, huku Christian Pulisic akielekea Old Trafford. (Daily Mail).
Kocha wa Barcelona Xavi anasema hatma ya Aubameyang kwenda Chelsea iko mguu ndani mguu nje.
“Hatujui nini kitatokea. Kwa sasa ni mchezaji wetu, ni mchezaji muhimu lakini mazingira yataeleza”.
“Kwa sasa si Auba au Memphis aliyeondoka... kipaumbele kwa sasa ni kukamilisha usajili wa Koundé (Laliga)”. (Romano)
Klabu ya Serie A, Lecce imeanza mazungumzo na Barcelona kwa ajili ya Samuel Umtiti.
Mazungumzo yanaendelea na huenda yakafikia hitimisho siku za mwisho dirisha la usajili. @SkySport
Nia ya Barcelona ya kumnasa Marcos Alonso wa Chelsea 'imeingia maji' kutokana na kuzongwa na ukata. Ni mpaka kuuzwa kwa wachezaji wake kadhaa ili kuweza kusajili wengine. Jana Klabu hiyo ilipokea ofa ya 15mil kutoka Chelsea kwa ajili ya mshambuliaji wake, Pierre-Emerick Aubameyang .
Memphis Depay kuvunja mkataba na Barcelona wiki inayokuja. Juventus wanaandaa kumsajili kwa mkataba wa miaka 2