Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi kubwa tano za soka Ulaya jioni hii (19.08.2022)
Kocha wa Arsenal Mikel Arteta amesema mshambuliaji wa pembeni wa timu hiyo, Bukayo Saka, anakaribia kusainia mkataba mpya.
“Nina imani kubwa kwamba upande wetu na upande wa Bukayo tuko pamoja- kilichosalia ni kuweka kwenye maandishi tu”, alisema. (Romano via Arsenal.com)
Arteta anasema pia kwa sasa klabu hiyo inajielekeza zaidi kuangalia mustakabali wa wachezaji wake kabla ya kufikiria kusajili wapya katika muda wa usajili uliobaki.
"Anapaswa kuwa mchezaji sahihi, tunataka kusajili mchezaji wa kiwango cha juu, sio mchezaji tu."
Kiungo wa Real Madrid, Casemiro asubuhi leo amewaaga wachezaji wenzake wa klabu hiyo baada ya kukubali kujiunga na Manchester United. Kocha wa Madrid, Carlo Ancelotti amethibitisha pia asubuhi kwamba Mbrazil huyo anakaribia kuondoka Bernabéu. (Skysport)
Mtendaji mkuu wa Borussia Dortmund Hans-Joachim Watzke amepuuzilia mbali taarifa kwamba klabu hiyo inaweza kumsajili Cristiano Ronaldo.
Kufuatia taarifa zilizotolewa na gazeti la BILD la Ujerumani lililosema kwamba Dortmund wanaweza kumsajili mshambuliaji huyo wa Manchester United, Watzke alisema: “nampenda, ukweli ni wazo zuri - kumuona Cristiano akicheza Signal Iduna Park. Lakini hakuna mkataba wowote tulioingia, kwa maana hiyo tuache kuzungumzia hilo." (Sky sport football)
Kocha wa NewcastleEddie Howe imeiambia Real Madrid isahau kuhusu jaribio lake la kumsajili Bruno Guimaraes kutoka Tyneside kufuatia tetesi kwamba imeelekeza nguvu kumsajili.
Mbrazil huyo mwenye miaka 24, alisajiliwa kwa ada ya £40m mwezi Januari akitokea Lyon, akionekana kama mbadala wa kiungo wa Madrid, Casemiro anayeelekea Manchester United.
End of Unaweza kusoma pia