Tetesi kubwa tano za soka Ulaya jioni hii (20.08.2022)

Maguire

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Maguire

Chelsea wanamtaka kweli Harry Maguire. Tetesi zimeendelea leo baada ya jana Chelsea kuwasiliana na Man Utd kuona kama kuna uwezekano kwa nahodha huyo kuhamia Chelsea, huku Christian Pulisic akielekea Old Trafford. (Daily Mail).

Kocha wa Barcelona Xavi anasema hatma ya Aubameyang kwenda Chelsea iko mguu ndani mguu nje.

“Hatujui nini kitatokea. Kwa sasa ni mchezaji wetu, ni mchezaji muhimu lakini mazingira yataeleza”.

“Kwa sasa si Auba au Memphis aliyeondoka... kipaumbele kwa sasa ni kukamilisha usajili wa Koundé (Laliga)”. (Romano)

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

Mwisho wa X ujumbe

Klabu ya Serie A, Lecce imeanza mazungumzo na Barcelona kwa ajili ya Samuel Umtiti.

Mazungumzo yanaendelea na huenda yakafikia hitimisho siku za mwisho dirisha la usajili. @SkySport

Umtiti

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Umtiti

Nia ya Barcelona ya kumnasa Marcos Alonso wa Chelsea 'imeingia maji' kutokana na kuzongwa na ukata. Ni mpaka kuuzwa kwa wachezaji wake kadhaa ili kuweza kusajili wengine. Jana Klabu hiyo ilipokea ofa ya 15mil kutoka Chelsea kwa ajili ya mshambuliaji wake, Pierre-Emerick Aubameyang .

Alonso

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Alonso

Memphis Depay kuvunja mkataba na Barcelona wiki inayokuja. Juventus wanaandaa kumsajili kwa mkataba wa miaka 2

Depay

Chanzo cha picha, Getty Images