Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 20.11.23

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Antoine Griezmann

Manchester United wako tayari kuongeza mara tatu mshahara wa Antoine Griezmann katika jitihada za kumsajili fowadi huyo wa Ufaransa, 32, kutoka Atletico Madrid mwezi Januari. (El Nacional, via Mundo Deportivo)

Juventus wanaweza kuwa tayari kumuuza winga Mwingereza Samuel Iling-Junior, 20, ambaye amekuwa akilengwa na Tottenham, katika dirisha la uhamisho la Januari. (Football Insider)

Aston Villa wanatafuta uwezekano wa kumnunua mshambuliaji wa Athletic Bilbao na Ghana Inaki Williams, 29 Januari. (Football Insider)

Mshambuliaji wa Ureno Bruno Fernandes, 29, amethibitisha kujitolea kwake kuendelea kuichezea Manchester United licha ya uvumi unaomhusisha na kuhamia Saudi Arabia. (90min)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Bruno fernandes

Tottenham na Chelsea wana nia ya kumnunua Antonio Nusa anayelengwa na Fulham, 18, mshambuliaji wa Norway ambaye anawika sana katika klabu ya Club Brugge. (Football Insider)

Newcastle United inaweza kurejea tena kumnunua mshambuliaji wa Paris St-Germain Mfaransa Hugo Ekitike, 21, mwezi Januari. (Football Insider)

Barcelona watafanya uhamisho wa kumsajili kiungo wa kati wa Uhispania Martin Zubimendi, 24, ambaye anahusishwa na Arsenal, kutoka Real Sociedad msimu ujao. (Sport - in Spanish)

Roma wako tayari kufikiria ofa kwa beki wa kati wa zamani wa England Chris Smalling, 33, mwezi Januari. (Gazzetta dello Sport - in Italian)

AC Milan watajaribu kuimarisha safu yao ya ushambuliaji mwezi Januari na wanaweza kumnunua fowadi wa Lille na Canada Jonathan David, 23. (Gazzetta dello Sport - in Italian)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Leroy Sane

Barcelona na Real Madrid wanafikiria kumnunua winga wa Bayern Munich na Ujerumani Leroy Sane, 27. (Sport - in Spanish)

Real Madrid wanafikiria kumsajili mshambuliaji mwengine kwa mkopo au wa kudumu mwezi Januari baada ya Vinicius jnr, 23, kuumia akiwa na timu ya taifa ya Brazil, huku mshambuliaji wa RB Leipzig na Ujerumani Timo Werner, 27, akilengwa. (Sport - in Spanish)

Barcelona wanaweza kupokea hadi euro 5m (£4.4m) kama fidia baada ya kiungo Gavi, 19, kuumia akichezea Uhispania (Mundo Deportivo - in Spanish)

Wachezaji wa Ligi ya Premia wanaoitwa 'Big Six' wametakiwa kulipa zaidi 'kifurushi cha uokoaji' kwa piramidi ya soka ya Uingereza baada ya Everton kukatwa pointi 10. (Telegraph - subscription required)

Imetafsiriwa na kuhaririwa na Seif Abdalla